Header Ads

Responsive Ads Here

BARABARA DAR SASA KUJENGWA KISASA,WATAKAOGUSWA NA MRADI HUO KUANZA KULIPWA KESHO


ME1
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipata maelezo mafupi kutoka
kwa baadhi ya Wananchi kuhusu maeneo ambayo miundombinu yake imekuwa
kero kwa wananchi,ikiwemo makaravati yaliyoziba na mitaro

ME2
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji
wa wilaya ya Kinonondi akizungumza na baadhi ya wananchi walioko kwenye
kituo cha daladala cha Simu 2000 
ME3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji
wa wilaya ya Kinonondi wakikagua miondombnu mingine ikiwemo madaraja na
makaravati yaliyoziba,ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho 
ME5
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji
wa wilaya ya Kinonondi wakikagua barabara ya Makumbusho mapema leo
jijini Dar.Picha na Emmnanuel Masaka-Globu ya Jamii.
…………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa
fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa
maeneo yasiyopangwa DMDP,ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho
sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara.
Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara,Mabonde ya Mito, Ujenzi wa
Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba
vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu
kiasi cha Shilingi Billion 230.
Miongoni mwa Barabara  zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel
hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea
Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200,
Kilungule na MMK.
Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.Amewataka
wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri
kwa kutafuta makazi bora sehemu nzuri zaidi na pia kufanyia shughuli
zingine za kimaendeleo zitakazo waingizia kipato.
Aidha Makonda  amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa
kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za
kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.Hata hivyo amesema
Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili
kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la
Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.
Makonda  amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na
kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile
anachostahili bila usumbufu.

No comments