Header Ads

Responsive Ads Here

AWOTTA Yaadhimisha Miaka 6 Na Malengo Makubwa ya Kusonga Mbele


AWOTA 3
Mwenyekitiwa Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA),Mary Kalikawe (katikati)  akisisitiza jambo kwa wanachama (hawapo pichani) wakati wa mkutano mkuu wa mwaka  ulioambatana na sherehe za kutimiza miaka sita ya chama hicho zilizofanyi jijini Dar es Slaam leo.Kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Devotha Mdachi na Katibu wa  chama hicho, Agnes Rwegasira .

AWOTA 10
Katibu Mkuu  wa   Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) , Agnes Rwegasira  akisisitiza jambo kwenye semina hiyo. iliyofanyika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) jijini Dar es Salaam
AWOTA 8
Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi.  Fatma s. Mchumo(kushoto) akitoa mchango kwenye semina hiyo
AWOTA 7
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake nchini Tanzania Bi. Jacqueline Maleko. (TWCC ) kulia, akiongea  wakati wa semina hiyo
AWOTA 1
Mkuu wa idara , Sera na Mpingo wa Wizara ya Maliasili naUtalii Tanzania, Dorothea Masawe (katikati) Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (wapilikushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Devotha Mdachi (wa tatu kutoka kulia) wakikata  keki ya kuadhimisha miaka 6 ya  AWOTTA.
AWOTA 9
Baadhi ya wanachama  na wafanyakazi wa chama cha   Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) wakiwa kwenye mkutano Mkuu wa Mwaka  uliaoambatana na sherehe za kutimiza  miaka sita tangu kuanzishwa kwa chama hicho. Wakati wa hafla  na semina iliyofanyika katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam
………………………….
Wakati serikali ya awamu ya tano imejipanga kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na kuimarisha zaidi sekta ya viwanda,Wanawake wanaojishughulisha na utalii kupitia umoja wao unaojulikana kama Association of Women in Tourism Tanzania   (AWOTTA) umeweka mikakati mikubwa ya kuhakikisha  inatumia fursa zilizopo kukuza sekta ya utalii.
Akiongea wakati wa mkutano wa  mkuu wa mwaka, hafla ya kuadhimisha miaka 6 ya umoja huo sambamba na semina ya kujadili changamoto na kuweka mikakati iliyofanyika jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa AWOTTA,Mary Kalikawe,aliipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais,Dk.John Magufuli,kwa jitihada inazofanya  kukuza uchumi kwa nchi kupitia sekta  mbalimbali.
Kalikawe alisema kuwa katika kipindi cha miaka 6 tangu ianzishwe AWOTTA imefanikiwa kwa kuwaunganisha wanawake wanaofanya biashara ya utalii hapa nchini kwa upande wa bara na visiwani na aliwataka akina wanawake wengi kujitokeza kujiunga na umoja huu kwa kuwa umoja ni nguvu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali kisekta.
Alibainisha  baadhi ya changamoto zinazokwamisha wanawake kuendesha shughuli za utalii ni kutokuwa na mitaji ya kutosha,kodi nyingi na kubwa zinazotozwa na serikali katika  sekta hiyo,na wananchi na wadau wengi kutokuwa na ufahamu kuhusiana na sekta hii japokuwa inachangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa na aliiomba serikali kusaidia kukabiliana na changamoto hizo hili sera ya Tanzania ya viwanda iende sambamba na fursa za kukuza utalii nchini.
Kwa upande wake,Afisa Mwandamizi kutoka kitengo cha sera na Mipango, Dorothea Masawe ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh.Ramo Makani katika maadhimisho hayo aliipongeza AWOTTA kwa kazi nzuri inayofanya ya kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza sekta ya utalii na aliahidi kuwa serikali itafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi hiyo “Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na AWOTTA katika kukuza utalii nchini,inawapongeza kwa kutimiza miaka 6 na itaendelea kufanya kazi nanyi bega kwa bega”.Alisisitiza.

No comments