Header Ads

Responsive Ads Here

AUAWA KISA MABISHANO YA MAKALIO YA MWANAMKE-RPC SHANNA


SHANA
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna ,akionekana akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari Mkoani hapo,kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisini kwake
.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani ,linamshikilia Ramadhani Habibu ,mkazi wa kijiji cha Vilabwa, wilaya ya Kisarawe, kwa kudaiwa kumchoma kisu mwenzake chanzo kikiwa ubishani wa makalio ya mwanamke aliyepita njia .
Kamanda wa polisi mkoani hapo ,Jonathan Shanna alieleza mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa kosa la mauaji .
Alisema Ramadhani anadaiwa kumuua Emmanuel Nassor (26) kwa kumchoma na kisu kifuani baada ya kutokea ubishi kati yao kuhusu ukubwa wa tako la msichana aliyewapita wakipiga soga kijiweni.
“Kuna mdada alipita sasa marehemu na mtuhumiwa walikuwa na wenzao kijiweni wakaanza kuzozana kuwa yule mdada ana Chura ,wengine wakasema la kawaida ” 
Kamanda Shanna ,alisema ubishi ulikuwa mkubwa ndipo Ramadhani kwa hasira,akakimbia nyumbani kuchukua kisu alichokitumia kumchoma mwenzake hadi kumuua.
Alisema mtuhumiwa alikimbia ambapo siku ya sept 27 majira ya saa 2.30 asubuhi aikamatwa .
Kamanda huyo ,aliwaasa vijana kuacha tabia ya kupoteza muda vijiweni badala ya kujishughulisha kimaendeleo .

No comments