Header Ads

Responsive Ads Here

ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili
kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa
kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa
David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .


Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili
kulia) akipata  maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho

Waziri
wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua
mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya
binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za
Tanzania,Malawi
,Burundi na Somalia Bella Bird.
Filbert
Rweyemamu,Arusha
Benki ya
Dunia imetoa Sh 200 Milioni  ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi
zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya
kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu.
 


Akizungumza
katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia
kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao
watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.

Alisema
kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika
masuala ya
utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya
taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili
vilivyopo katika Chuo cha Kilimo
cha Sokoine(Sua).
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds
alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana
utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.
Bella alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia
katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira kwa
vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana vyema na
serikali .
Makamu wa
Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa
mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa
hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Godfrey  Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa
wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu
waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi
huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

No comments