Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKABIDHIWA RIPOTI TATU NA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA


akipokea
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea moja ya Ripoti tatu alizokabidhiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki, kushoto ni Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome.

AKIPOKEA RIPOTIKABUDI HOTUBA
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi akizungumza na maofisa wa Tume na wale wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa makabidhiano ya Ripoti.
KYUKI
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti tatu kwa Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi.
AKIWA NA WAKUU
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi akiangalia Ripoti alizokabidhiwa na Tume ya Kurekebisha Sheria, wengine pichani ni Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome (wa pili kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume Casmir Kyuki (kushoto kwa waziri), Katibu Msaidizi wa Tume Agnes Mgeyekwa (Kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Katiba na Sheria Mercy Mrutu.
PICHA PAMOJA
Prof Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Wizara na wale wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakati wa tukio la kukabidhiwa Ripoti.
………………………
NA Munir Shemweta LRCT
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi leo amepokea Ripoti tatu zilizofanyiwa kazi na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Ripoti alizokabidhiwa Prof.  Kabudi ni Mapitio ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu, Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Huduma za Jamii kwa Wazee na Ripoti ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazohusu Haki za Walaji na Watumiaji Bidhaa na Huduma.
Mkabidhiano ya ripoti hizo yamefanyika leo baina ya Waziri wa Katiba na Sheria na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ripoti hizo Prof. Kabudi ameipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa kazi nzuri iliyoifanya ya kufanya mapitio na hatimaye kuja na mapendekezo yanye lengo la kuboresha sheria husika.
Amesema, Tume ni taasisi muhimu sana katika kufanya mapito ya sheria mbalimbali na kuweka bayana kuwa, kuna haja ya mapitio ya sheria mbalimbali yanayofanyika nchini kuishirikisha Tume ambayo ina jukumu la kufanya hivyo kulingana na sheria iliyoianzisha.
Akielezea Mapitio ya Sheria inayosimamia Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Prof. Kabudi amesema kutokana na umuhimu wa sheria hiyo atahakikisha mapendekezo ya sheria hiyo yanafanyiwa kazi haraka ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa katika kikao kijacho cha Bunge la mwezi Septemba.
Kuhusu Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee, Waziri wa Katiba na Sheria ameieleza ripoti hiyo kuwa ni muhimu sana hasa ikizingatiwa wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile huduma za afya na  pensheni na kusisitiza kuwa kila mtu ni mzee mtarajiwa.
Aidha, Prof Kabudi amezitaka Taasisi zote zilizo chini ya wizara ya Katiba na Sheria kushirikiana katika kazi zake hususan katika mapitio ya sheria mbalimbali ili kuja matokeo chanya katika sekta ya sheria.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria anzania Bw. Casmir Kyuki alisema Tume yake imefanya utafiti wa kina wakati wa kupitia sheria hizo tatu ikiwa ni pamoja  kutembelea maeneo mbalimbali nchini lengo likiwa ni kupata maoni kutoka kwa wadau  ambao ni taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi wa kawaida.
Munir Shemweta
Afisa Habari
0655 959465/0786249844
11 Agosti, 2011

No comments