Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI MKUU AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KWENDA KUWATUMIKIA WANANCHI VIJIJINI


VIJI
Na Tiganya Vincent-Tabora
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wote wa umma kuondoka maofisa na kwenda vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambazo yanasababisha wasiendelee.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana wakati akiongea na watumishi wa Wilaya ya Uyi mkoani Tabora.
Alisema kuwa wakisha kuwasiliza wananchi warudi Ofisi kwa ajili ya kujipanga namna ya kutatua kero na matatizo ya wananchi ambayo yanakwamisha juhudi zao ya kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote na hivyo imetoa dhamana kwa watumishi wa umma wafanye kazi karibuni kwa kwenda vijijini  ili kuwatumikia Watanzania wote.
Aidha alionya kuwa Serikali hii haitawavumilia watumishi wa umma wenye tabia za urasimu katika kuwatumikia na kutatua kero mbalimbali za watanzania.
“Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote wa umma ambayo mwananchi anakwenda kwake kwa mara ya kwanza kueleza shida yake kisha anamwambia mwananchi arudi kesho na anaporudi kesho , anambia tena arudi kesho …..mwisho mwananchi anaanza kukata tamaa ya kusaidiwa tatizo lake” alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema kuwa mwanachi anapofika katika Ofisi za Umma kwa ajili ya kutatuliwa tatizo lake asaidiwe haraka bila kuzungushwa zungushwa ili aone Serikali yake ipo kwa ajili ya kumsaidia.

No comments