Header Ads

Responsive Ads Here

WATHAMINI WASIO WAADILIFU KUKIONA


mtha
Serikali yakemea vitendo viovu vinavyofanywa na wathamini kuhusu uthamini wa fidia na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria watumishi wasio waaminifu ikiwemo kuwanyang’anya leseni zao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha katika kikao kazi cha wathamini wa manispaa zote za Dar es Salaam na wale wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi.
Mugasha amesema wakati wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha lililobaki ni kubadilika na kufanya kazi kwa uadilifu ili kurudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.
“Mimi baada ya kuteuliwa kuwa Mthan=mini Mkuu wa Serikali nimeamua kuhakikisha wathamini wanarudisha imani na kutenda haki kwa wananchi,”alisema Mugasha.
Ameongeza kuwa migogoro ya uthamini inabidi iishe mara moja kwani wananchi wamechoshwa na vitendo vibaya walivyokuwa wakifanyiwa na wathamini.
Mugasha amewataka wathamini wajisajili kwani ambaye hajasajiliwa hataruhusiwa kufanya kazi ya uthamini vinginevyo atafute kazi nyingine.
Amezitaka manispaa zote nchini kuwa na kanzidata zake kuhusu masuala ya uthamini na ziwe zinauhishwa mara kwa mara, na kwa kufanya hivyo malalamiko ya uthamini yatapungua ama kuisha kabisa.

No comments