Header Ads

Responsive Ads Here

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KISASA KATIKA KILIMOMkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.(Picha na Pamela Mollel)
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na wananchi hili katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.
Wananchi wakiwa wanaangalia bwawa la samaki katika banda la halmashauri ya mji wa Babati katika maonyesho ya nane nane

WATANZANIA wameshauriwa kutumia teknolojia za kisasa katika kada za kilimo,mifugo na uvuvi ili kujipatia ajira na kipato na hatimaye kukuza lengo la uchumi wa viwanda.

Ushauri huo ulitolewa jana jijini Arusha na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na gazeti hili kwenye maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.

Luther alisema kuwa endapo watanzania wataamua kuwekeza nguvu zao katika teknolojia hizo ikiwemo ufugaji wa samaki wataweza kujiingizia kipato katika ngazi ya kaya kupitia samaki watakazozalisha.

"Ufugaji wa samaki kisasa si lazima uwe na eneo kubwa hata eneo dogo nyumbani kwako unaweza ukafuga ama hata katika simtank,madyaba ama pipa ili mradi eneo hilo liwe na hewa pamoja na usafi wa mazingira ya maji ya kuhifadhia samaki wako.

"Mradi huu unawezesha ajira na thamani ya utengenezaji wake ni ndogo sana ukizingatia na faida utakayoipata baadae hivyo vijana wachangamkie hii fursa kuliko kusubiri ajira serikalini"alisema Luther.

Aidha aliwataka watanzania kuwekeza katika kilimo cha mazao yenye thamani ikiwemo kilimo cha uyoga, mbogamboga za majani,matunda na mizizi kwa kusindika mazao hayo ili kuendeleza soko lake na kujipatia kipato.

imu wa mavuno mazao yanakuwa mengi na mengine yanaweza kuharibika lakini yakiweza kuongezewa thamani kwa kukaushwa hasa mbogamboga tunaweza kuendelea kuwa na soko hili na kujiongezea kipato.

"Mfano zao la uyoga linaweza kuendelea kupatikana katika soko kwakuwa umekaushwa tofauti na ukiwa mbichi kwani huaribika kwa haraka

No comments