Header Ads

Responsive Ads Here

WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI TABORA WATAKIWA KUJIPANGA ILI WAACHE KUENDELEA NA UKOPAJI WA MBOLEA.


Picture 013
Na Tiganya Vincent-Tabora
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim ametoa wito kwa Wakulima wa  tumbaku mkoani Tabora kuanza kujipanga ili waanze kilimo cha zao hilo kwa kunununua mbolea kwa kutumia fedha zao badala ya kuendelea kutegemea mbolea za mkopo kupitia vyama vya msingi.

Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana katika maeneo mbalimbali wilayani Uyui wakati akiwahutubia wananchi.
Alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakulima hilo kuwa na huru hata wakati wa kupanga bei ya zao wanapokwenda kuwauzia wanunuzi wa tumbaku.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa tabia ya kuendelea kusubiri mbolea ya mkopo inawafanya wakulima wengi washindwe kusonga mbele kwa sababu pesa nyingi inakwenda katika kulipia deni la mbolea.
“Ndugu zangu wakulima  watumbaku ni vema kuanzia sasa mkaanza kujipanga kwa msimu ujao wa kilimo kwa kununua mbolea kidogo kidogo ili ikiwezekana ulime kwa kutumia mbolea ulionunua mwenyewe……..hali hii itakufanya uwe uhuru hata wa kuamua bei unayotaka” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Alisema kuwa ni wakulima wakaanza kwa kununua kidogo dogo mbolea ya tumbaku kupitia mapato yanayotokana na mauzo ya tumbaku yao kama hatua ya kuelekea katika kujikomboa na kuondokana na utegemezi wa mbolea za mikopo ambayo zimewaingiza katika matatizo mbalimbali ikiwemo kuwa siku nyuma kimaendeleo.
Aidha Waziri Mkuu amepiga marufuku Kampuni zinazonunua tumbaku hapa nchini kununua zao hilo kutoka kwa Mkulima kwa njia ya fedha ya Kimarekani (Dola) na kusema kuwa vitendo hivyo ndio vinasababisha unyonyaji wakulima.
Alisema tumbaku yote kuanzia sasa itakuwa ikinunuliwa kwa fedha ya kitanzania na sio vinginevyo.
Mhe. Majaliwa alisisitiza kuwa wakulima wengi hajui dola jambo ambalo limefanya viongozi wengi wakiwemo wa vyama vya msingi kumibia mkulima.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema kuwa mtu akayekamatwa ananunua tumbaku ya mkulima kwa njia ya vishada Serikali haitamuachia na kama atakuwa ana chombo cha usafiri kitashikiliwa na Polisi ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kuwavizia wakulima walime kisha wao waende kurubuni na kununua tumbaku yao kwa nia ya ulanguzi.
Alisisitiza kuwa tumbaku yote itauzwa kupitia Vyama vya Msingi na sio vinginevyo na mtu yoyote atakayekutwa akiuza tumbaku nje ya utaratibu wa Serikali atachukuliwa hatua kali.

No comments