Header Ads

Responsive Ads Here

Wafanyakazi Bora Muhimbili Watunukiwa Vyeti vya ufanyakazi bora


001
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika tafrija ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora wa mwaka 2017.  Kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali Watu wa hospitali hiyo, Makwaia Makani na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege.

002
Baadhi ya wafanyakazi wakimzikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru kabla ya wafanyakazi bora kukabidhiwa vyeti.
003
Mmoja wa wafanyakazi bora, Abdallah Iddi akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru.
004
Dk. Methew Kalanga akiwa na Mkurugenzi mtendaji baada ya kukabidhiwa cheti.
005
Mfanyakazi bora, Mwajuma Kisengo akikabidhiwa cheti.
006007
Baadhi ya wafanyakzi wakicheza muziki katika hafla hiyo.
008
Wafanyakazi bora wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru.
…………………………………………………………………………
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amewatunuku vyeti wafanyakazi 49 wa hospitali hiyo baada kuchaguliwa kuwa wafanyakazi bora.
Shughuli ya kuwakabidhi vyeti pamoja na zawadi nyingine ilifanyika katika hospitali hiyo, huku Mkurugenzi akiwataka wafanyakazi wasimbweteke bali waongeze bidii ili kuiwezesha hospitali kutoa huduma bora za kibingwa.
Akizungumza katika tafrija ya kuwatunuku vyeti, Mkurugenzi aliwaeleza kwamba uongozi wa hospitali unafanya juhudi kubwa ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi hivyo wasimwangushe katika kufikia malengo ya kutoa huduma bora za kibingwa.
Katika risala ya wafanyakazi ambayo ilisomwa na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege, wafanyakazi  walimpongeza Profesa Museru pamoja na uongozi wa hospitali hiyo kwa juhudi kubwa za kukarabati majengo na kununua vifaa tiba kwa lengo la kuboresha huduma za afya.
“Pamoja na pongezi hizo, tunakuomba sana uboreshe viwango vya zawadi kwa wafanyakazi bora watakaochaguliwa kipindi kingine,” amesema Chimwege.

No comments