Header Ads

Responsive Ads Here

WADAU WAENDELEA KUUNDA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA


mada
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shilingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.

Makonda amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi  20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.
Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza  uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.
Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi  viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.
Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.
“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.
Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Dar es Salaam

No comments