Header Ads

Responsive Ads Here

ULINZI WA KIMATANDAO KUIMARISHWA NCHINI ILI KULINDA MIFUMO

>
> Na Jonas Kamaleki – MAELEZO
>
> Serikali kushirikiana na sekta
> binafsi wanaweza kujenga msingi wa kitaifa katika kuimarisha
> Usalama katika ulimwengu mzima kwa ujumla na kudondokana na
> uhalifu wa kimitandao.

>
> Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
> na Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Matt
> Sutherland wakati wa ufunguzi wa Warsha ya masuala muhimu
> katika kuweka miondombinu ya kiusalama katika mitandao.
>
> Sutherland amesema kuwa uhalifu wa
> kimitandao haungalii mipaka ya nchi bali unaweza kutokea
> mahali popote na wakati wowote. Alisisitiza hilo amesema
> kuwa mwezi Mei mwaka huu shambulio la kimtandao lilipiga
> mifumo karibu nchi 100 Duniani..
>
> “Katika shambulio hilo, Uingereza
> tuliathirika sana hasa katika sekta ya Afya ambapo kompyuta
> katika Hospitali nyingi zilishindwa kufanya kazi na
> kusababisha madaktari kushindwa kupata taarifa za wagonjwa,
> ” alisema Sutherland .
>
> Ameongeza kuwa Septemba mwaka jana
> wakati lilipotokea tetemeko la ardhi Mkoani Kagera,
> Uingereza ilikuwa mstari wa mbele katika kurejesha
> miondombinu ya shule ya sekondari Ihungo kwani katika tukio
> hilo waliotharika zaidi ni wanafunzi.
>
> Akiongelea suala la kiusalama, Naibu
> Balozi huyo amesema kuwa katika Mkutano wa Kilele
> utakaofanyika mwakani utangalia masuala mbalimbali ya
> kiusalama ikiwemo kupambana na ugaidi wa kimataifa,uhalifu
> wa makusudi, mashambulio ya kimtandao utumwa mambo leo
> na vitisho vya demokrasia.
>
> Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Warsha,
> Dkt. Martin Koyabe kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya
> ya Madola (CTO) amesema kuwa lento la Warsha hii ni
> kuwawezesha watumishi wa umma na wa sekta binafsi kufahamu
> miondombinu ya kiusalama katika sekta muhimu za kiuchumi ili
> kuleta maendeleo nchini.
>
> Aidha, Dkt Koyabe amesema kuwa warsha
> hii inakusanya watumishi pamoja ili kuwa uelewa wa kuainisha
> maeneo muhimu ya kiuchumi yanayotakiwa mifumo yake ya
> kimitandao kulindwa ili uchumi usiathirike endapo mifumo
> hiyo inashambuliwa.
>
> “Serikali ni muhimu kutunga sera,
> sheria na kanuni za kuweka ulinzi wa kimitandao ili
> tusiathirike wakati shambulio linapotokea,” alisema Dkt.
> Koyabe
>
> Ameongeza kuwa zipo changamoto kadhaa
> katika kutekeleza programu za ulinzi wa kimitandao.
> Amezitaja changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa bajeti, uhaba wa
> wataalaam na utaalaam katika eneo la ulinzi wa kimitandao.
>
> Warsha hii ni mwendelezo wa juhudi za
> Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na CTO katika
> kukamilisha Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Kimitandao
> (National Cyber Security Strategy).
>

No comments