Header Ads

Responsive Ads Here

TRA YAKABIDHI UENYEKITI WA EARATC KWA OBR-BURUNDI

5
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake EARATC Bw. Michael Muhoja kutoka TRA akikabidhi ngao na nyundo kama ishara ya kumkabidhi vitendea kazi mwenyekiti mpya Bi. Martine Nibesumba kutoka OBR Burundi.

4
Mwenyekiti mpya Bi. Martine akifungua kikao kazi cha EARATC mara baada ya kukabidhiwa rasmi uenyekiti.
2
Mwenyekiti mpya wa EARATC Bi. Martine Nibesumba kutoka OBR-Burundi
1
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja
…………………………..
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi uenyekiti wa kamati ya ufundi ya masuala mbalimbali ya utekelezaji katika Mamlaka za Mapato zilizopo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Revenue Authorities Technical Committee). Katika mkutano wa 80 unaoendelea tangu tarehe 14 hadi 18 Agosti, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha International Conference Centre jijini Arusha ambapo Tanzania imekabidhi nafasi hiyo kwa nchi ya Burundi.
Nafasi ya uenyekiti ilikuwa inashikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango Bw. Michael Muhoja nafasi ambayo ameishikilia kwa muda wa mwaka mmoja. Katika kipindi hicho ameweza kufanikisha utekelezaji wa majukumu yote 13 yaliyoanishwa kwenye mpango kazi wa kamati hiyo ambayo inajumuisha wataalamu kutoka idara mbalimbali za mamlaka za mapato kutoka Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania.
Bw. Muhoja amekabidhi uenyekiti kwa Bi. Martine Nibasumba kutoka Mamlaka ya Mapato ya Burundi ambapo naye atatumikia kwa mwaka mmoja na atasimamia utekelezaji wa  maazimio ya kikao hiki ambayo yataidhinishwa na Makamishna Wakuu wa mamlaka za mapato katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kikao hiki ni cha siku tano mfululizo kitapokea ripoti kutoka kwa Wakuu wa Idara wa kila nchi mshiriki kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali walizokubaliana katika vikao vilivyopita na kupeana mrejesho wa hatua mbalimbali walizofanya katika kuhakikisha kuwa shughuli za mamlaka za mapato katika nchi za afrika mashariki zinatekelezwa kwa ajili ya maendeleo ya ukanda mzima.
 Akikabidhi ngao pamoja na nyundo kama alama ya vifaa vya kutendea kazi ya uenyekiti, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw. Muhoja, amesema anakabidhi wadhifa wa uenyekiti akiwa na amani kwa kuwa ametekeleza majukumu yake na kuwashukuru wajumbe wote kwa kumpa ushirikiano mkubwa wakati wa utekelezaji.
“Napenda kuwashukuru wajumbe wote wa kamati ya ufundi kutoka nchi zote, na sasa nakabidhi rasmi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya kutoka Burundi,” amesema Bw. Muhoja.
Aidha, Bi. Martine, amepokea nafasi hiyo ambayo inamfanya aongoze utekelezaji wa majukumu mbalimbali kama yatakavyoainishwa na kamati pamoja kuidhinishwa na kikako cha Makamishna Wakuu kwa ajili ya utekelezaji.
Katika Mkutano huu wa 80 nchi zilizoweza kuhudhuria ni pamoja na wajumbe kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na Tanzania, isipokuwa Sudan Kusini ambayo hawakuhudhuria.

No comments