Header Ads

Responsive Ads Here

TPB YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA JIJINI TANGA”

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba Mashingi akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo


 Afisa
Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba
Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki
wa Kongamo hilo la Biashara.
AFISA Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia huduma wanazozitoa hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua wigo wa biashara zao. 

Moshingi aliyasema hayo leo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la
biashara lililofanyika katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dokta Harrison
Mwakyembe.

Kongamano hilo la biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN)
katika mkoa wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za
serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na
wasomi.
 

“Niwaambie tu huduma hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina
mbalimbali lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa
mara nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.
 
“Lakini pia nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani
Tanga lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali
tunazozitoa. 
 

“Kwani Benki yetu ya TPB imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua
shughuli zake za kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa
ujumla “Alisema Moshingi. 
 

Aidha pia alisema wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ta
tano  kuipeleka nchi kwenye uchumi wa
viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa vikiwemo vya mkoani
Tanga. 
 

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la
mafuta uliozinduliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao kama benki wapo tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments