Header Ads

Responsive Ads Here

TFF YAIFANYIA MAREKEBISHO NGAO YA JAMII WALIOICHUKUA SIMBA


 
Hatimaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii waliyoshinda Simba.
Simba walikabidhiwa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju 5-4 ya penalti, lakini ikawa na makosa katika maandishi.
Ngao hiyo ilikuwa imeandikwa, Community Sheild badala ya Community Shield.
Baada ya malalamiko kuwa makubwa, TFF iliomba Simba kuirudisha ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho na sasa hilo, limefanyika.
 

No comments