Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Yazindua Programu Ya Voyager Plant Optimization (VPO)


VPO TBL 2
Mkurugenzi wa shughuli za uzalishaji wa viwanda vya TBL Group, John Gouws,akiwapiga darasa wafanyakazi kuhusiana program hii mpya ambayo ikitumika ipasavyo itawezesha kupatikana matokeo makubwa.

VPO TBL 4Meneja wa kiwanda cha  Tanzania Breweries Limited (TBL),cha Ilala jijini Dar es Salaam,Calvin Martin,akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi huo.
VPO TBL 5
Meneja wa Afya na Usalama wa TBL,Renatus Nyanda, akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi huo.
VPO TBL 7
Baadhi ya wafanyakazi wakisikiliza kwa makini jinsi programu hiyo inavyofanya kazi.
…………………………
-Itaongeza ufanisi zaidi kwa viwanda vyake kuelekea Tanzania ya viwanda
Kampuni ya kutengeneza bia  Tanzania ya TBL imezindua programu ya uendeshaji wa shughuli zake kisasa zaidi na kuwezesha kufanya tathmini ya malengo inayojulikana kitaalamu kama Voyager Plant Optimization (VPO) lengo likiwa ni kuongeza tija na ufanisi wa viwanda vya kampuni vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya,na Arusha.
Programu hii ya kampuni mama ya TBL Group ya ABINBEV tayari inatumika katika nchi mbalimbali  duniani ambako inaendesha biashara zake na imeonekana kuleta mafanikio ya kupima malengo ambayo  kampuni imejiwekea na kuhakikisha biashara za kampuni zinaendeshwa katika mfumo unaofanana  popote  ambapo imewekeza.
Akiongea wakati wa uzinduzi  wake jijini Dar es Salaam,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Ilala,Calvin Martin,alisema kuwa Programu hii mpya inamhusu kila mfanyakazi wa kampuni kwa kuwa ili mafanikio yapatikane kunahitajika ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi wote na ndio maana kunatolewa  mafunzo ya ndani kwa lengo la kumuwezesha kila mfanyakazi wa kampuni kuuelewa vizuri na kuutumia.
Martin alisema kuwa mfumo huu mpya ni endelevu katika shughuli za  kila siku  za uendeshaji wa viwanda kwa lengo la kuongeza ufanisi  na kupunguza gharama za uzalishaji sambamba na  kuongeza ubora  wa bidhaa zinazozalishwa,kuimarisha usalama maeneo ya kazi na kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira.
VPO itafanikisha kupima ufanikishaji wa malengo tuliyojiwekea ikiwemo kupunguza gharama za matumizi ya uendeshaji na ikitumika ipasavyo itaweza kuleta mafanikio ndani ya kampuni kwa kuwa popote ambapo imetumika imeonyesha kuongeza ubora na ufanisi na kufanikisha malengo ya  kampuni  ambayo yako sambamba na malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) hususani katika maeneo ya utunzaji wa mazingira,matumizi mazuri ya maji na kuendesha viwanda kwa nishati mbadala zizizo na athari kwa mazingira”Alisema Martin.
TBL Group kwa kiasi kikubwa imefanikisha malengo mbalimbali ya kupunguza uharibifu wa mazingira ma matumizi  mazuri ya maji ambapo kwa upande wa maji  matumizi yamepungua  kutoka hectolita   za miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa wakati huo mifumo ya utakatishaji wa maji taka ikitumika lengo likiwa ni ktumia maji kidogo zaidi katika shughuli za uzalishaji na zisizo za uzalishaji.
Kwa upande wa matumizi ya nishati mbadala rafiki kwa mazingira  kampuni imeanza mkakati za kuzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya jua ambapo tayari zimeanza kufanya kazi katika kiwanda cha TBL Mbeya na  katika kiwanda cha mwanza tayari kinafanya uzalishaji kwa kutumia sehemu ya umeme unaozalishwa kutokana na teknolojia ya pumba za mpunga lengo kubwa likiwa ni kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa,kuzalisha nishati safi na endelevu vilevile, kupunguza gharama za kununua mafuta.

No comments