Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Group yang’ara tamasha la Usalama barabarani Dar


TBL 4
Rais msaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassani Mwinyi,akipata maelezo ya jitihada za kampuni ya TBL Group kupambana na ajali za barabarani kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo  Amanda Walter kwenye tamasha la usalama  barabarani lililofanyika  jijini Dar e salaam mwishoni mwa wiki (kulia mwenye kofia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mh.Hamad Masauni.

TBL 2
Daktari wa macho katika gari la Zahanati mwendo laTBL Group, Nestory Massawe (Kulia) akimpima macho mwananchi Omar Hussein wakati wa tamasha la usalama  barabarani katika uwanja wa Taifa anayeshuhudia (Kushoto) ni Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Amanda Walter
TBL 3
Baadhi ya madereva wa bodaboda wakipata mafunzo ya usalama barabarani kutoka kwa maofisa wa TBL wakati wa tamasha hilo
TBL 9
Rais Mstaafu,Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria tamasha hilo.
……………………………………………………………
-Kuendelea kuunga mkono kampeni za Usalama Barabarani
 
Kampuni ya TBL Group  imeeleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine nchini kuunga mkono kampeni za usalama barabarani lengo  likiwa ni kupunguza ajali nchini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya watu ,kuacha wananchi wengi wakiwa walemavu na kusababisha hasara mbalimbali.
 
Akiongea wakati wa tamasha  la Usalama barabarani 2017,lililoandaliwa na serikali   kupitia Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani na kufanyika  katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,alisema suala la usalama wa barabarani kampuni inalipa kipaumbele mkubwa na ndio maana imekuwa ikijihusisha nalo kama moja ya agenda ya kusaidia huduma za kijamii.
 
Alisema kuwa kampuni imekuwa moja ya wadau wakubwa wa kudhamini wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani mwaka hadi mwaka sambamba na kudhamini mafunzo,vitendea kazi na wafanyakazi wake kushiriki katika kutoa elimu  ikiwa ni ufanikishaji wa moja ya mkakati wa kampuni  wa kutokomeza  matukio ya ajali za barabarani na maeneo ya kazi.
 
Linapokuja suala la usalama kampuni inalizingatia kuanzia usalama wa ndani katika maeneo ya kampuni  hadi usalama wa barabarani kwa ajili ya watu wote na ndio maana tumekuwa tukiunga mkono kampeni hizi  ikiwemo kuwamasisha madereva wasiendeshe vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi”.Alisema Walter.
 
Aliongeza kuwa hivi sasa kampuni hiyo imekuja na mkakati mkubwa wa kuendesha mafunzo ya kuhamasisha jamii Unywaji wa Kistaarabu “Tukiwa kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi tunalo jukumu pia kuhamasisha jamii kutumia vinywaji hivyo vizuri ili utumiaji wake usilete madhara mengine kwenye jamii”
 
Mwaka jana TBL Group ilikuwa mmoja wa wadhamini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo iliwezesha idadi kubwa ya madereva kupima afya zao kupitia huduma ya Zahanati Mwendo pia imekuwa ikiendelea kudhamini kampeni hizo kwenye ngazi za mikoa ikiwemo kudhamini mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi.
 
Katika tamasha hilo gari la Zahati Mwendo la TBL Group lilikuwa moja ya kivutio kikubwa kwa wananchi walioudhuria ambapo  baadhi yao waliweza kupata huduma za ushauri wa kiafya na kupimwa macho.
 
Akiongea  baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya taasisi mbalimbali katika tamasha hilo,Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ali Hassan Mwinyi,aliwapongeza wadau wote ambao wanashiriki kampeni za kutokomeza matukio ya ajali nchini na kutoa wito kuwa serikali ikishirikiana na taasisi zisizo za kiserikali kukabiliana na changamoto  mbalimbali zilizopo kwenye jamii mafanikio yatapatikana kwa haraka na taifa kuzidi kusonga mbele kwa haraka.

No comments