Header Ads

Responsive Ads Here

TANGAZO KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA


MPI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI MOHAMMED R. MPINGA KUPITIA OFISI YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO MKOA WA MBEYA ANAWATANGAZIA WANANCHI NA WAKAZI WA MKOA WA MBEYA KUWA AMEANDAA BONANZA LA SIKU TANO [05] KUANZIA TAREHE 20/08/2017 HADI 25/08/2017 LITAKALOHUSISHA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI MKOANI HAPA.

BONANZA HILI LITAKUWA LIKIFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA FFU MBEYA KUANZIA SAA 08:30 MCHANA HADI SAA 11:30 JIONI. LENGO LA BONANZA HILI NI KUWAWEKA PAMOJA WATOTO WALIOPO SHULENI NA WATOTO WA MITAANI ILI KUWABADILI KIFIKRA.
WATOTO KUANZIA UMRI WA MIAKA 10 – 15 NDIO WATAKAOHUSIKA KATIKA BONANZA HILI. MICHEZO ITAKAYOSHINDANIWA NI MPIRA WA MIGUU, KUVUTA KAMBA, KUKIMBIZA KUKU, KUKIMBIA KWENYE GUNIA NA KUCHEZA KARATA.
MGENI RASMI WA BONANZA HILI ATAKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI MOHAMMED R. MPINGA.
KAULI MBIU YA BONANZA HILI NI “JUKUMU LA MALEZI YA MTOTO NI LETU SOTE, CHUKUA HATUA KATIKA KUMLINDA MTOTO”
NYOTE MNAKARIBISHWA.
Imesainiwa na:
 [MOHAMMED R. MPINGA –DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBMPIA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments