Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                      DAR ES SALAAM, 25 Agosti, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananch wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya majeshi yanayoanza tarehe               25 Agosti 2017. Sherehe hizi ni za kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo hufanyika kila mwaka tarehe 01Septemba, mwaka huu sherehe hizo zitaadhimishwa wakati Jeshi linatimiza miaka 53 tangu lilipo asisiwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza Marehemu Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere  Septemba Mosi 1964.
Mwaka huu 2017 maadhimisho hayo yatafanyika kwa wanajeshi kufanya shughuli mbalimbali kuanzia tarehe 25 Agosti 2017 hadi tarehe 31 Agosti 2017 na kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 01 Septemba 2017.Shughuli hizo ni pamoja na kufanya shughuli za huduma za kijamii katika maeneo jirani na vikosi vya Jeshi, Wanajeshi kuchangia damu salama katika hospitali mbalimbali nchini, kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa Dar es salaam huduma za tiba zitatolewa katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya tarehe 01 Septemba, aidha wanajeshi watafanya michezo mbalimbali na wananchi Pamoja na kushiriki kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii (Hospitali, Masoko, Mashule n.k) na pia watafanya michezo Shirikishi na jamii inayowazunguka.
Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni Wiki ya Majeshi na Afya yako.
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

No comments