Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 24.08.2017
  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMTEKA MTOTO WA MIAKA NANE (8) WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 23.08.2017 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA LUMALA KATA YA PASIANSI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, EMMANUEL KIRUMBAS, MIAKA 25, MKAZI WA MALAMPAKA MKOANI SHINYANGA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMTEKA MTOTO WAKIKE AITWAYE KHAILATI BASHIRI MIAKA 8, MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI ILOGANZALA, NA KUMPELEKA  KUSIKOJULIKA NA BAADAE  KUTUMA TAARIFA KWA NJIA YA SIMU KWAMBA APEWE FEDHA KIASI CHA MILIONI TATU  (TSH 3,000,000)  ILI AWEZE KUMRUDISHA MTOTO KWA WAZAZI WAKE, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.
INADAIWA KUWA TUKIO LA KUTEKWA MTOTO LILITOKEA TAREHE 21.08.2017 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA, INASEMEKANA KUWA BAADA YA MTOTO KUTOKA SHULENI ALIKWENDA NYUMBANI KWAO MTAA WA ILOGANZALA ANAPOISHI NA WAZAZI WAKE KUBADILISHA NGUO KISHA ALIONDOKA NA KUELEKEA KUSIKOJULIKANA. WAZAZI NA MAJIRANI WALIHANGAIKA KUMTAFUTA MTOTO HUYO BILA MAFANIKIO NDIPO WALIAMUA KUTOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
ASKARI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIZO WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI NYUMBANI KWA WAZAZI WA MTOTO NA KUSHIRIKIANA KUMTAFUTA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MWANZA. INADAIWA KUWA WAKATI WANAENDELEA NA MSAKO MTUHUMIWA WA UTEKAJI ALIPIGA SIMU KWA WAZAZI WA MTOTO AKIWATAKA WAMPATIE FEDHA KIASI CHA MILIONI TATU (TSH.3,000,000/=), ILI AWEZE KUMREJESHA MTOTO HUYO KWA WAZAZI WAKE.
POLISI WALIFANYA UPELELEZI AMBAO ULIPELEKEA KUKAMATA WATU WATANO NA BAADAE KUFANIKIWA KUMKAMATA MTEKAJI NYARA AMBAE ALIKUWA AKIHITAJI FEDHA TAJWA HAPO JUU. POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA UTEKAJI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WALIOSHIRIKIANA NA MTUHUMIWA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA UTEKAJI HUO BADO UNAENDELEA. MTOTO TAYARI AMEKABIDHIWA KWA FAMILIA YAKE AKIWA MZIMA NA AFYA NJEMA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI AKIWATAKA KUWA WAANGALIFU NA WATOTO DHIDI NA WATU WENYE NIA OVU DHIDI YAO. AIDHA PIA ANAWAOMBA WAMILIKI WA NYUMBA KUACHA TABIA YA KUWAPANGISHA NYUMBA/ CHUMBA WATU WASIOWAFAHAMU NA WASIOKUWA NA SHUGHULI YA KUELEWEKA KWANI WANAWEZA KUWAINGIZA KWENYE MATATIZO. PIA ANATOA ONYO KWA WALE WOTE WENYE TABIA CHAFU KWANI JESHI LA POLISI LIKO IMARA NA VIZURI LENYE UWEZO WA KUWAKAMATA HARAKA PALE TU WAKIFANYA VITU KAMA HIVI.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments