Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 17.08.2017
  • MTU MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE PAGALA WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 16.08.2017 MAJIRA YA SAA 17:30HRS KATIKA MTAA WA KITANGIRI KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMKE JINA BADO HALIJAFAHAMIKA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA 40 HADI 45 AMEKUTWA AKIWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE PAGALA HUKU UKIWA UMEFUNGWA KWENYE MFUKO WA SANDARUSI NA KUZUNGUSHIWA NGUO ALIZOKUWA AMEVAA MAREHEMU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI MWILI WA MAREHEMU ULIWEZA KUONEKANA MAHALI HAPO BAADA YA WATOTO WALIOKUWA WAKICHEZA ENEO HILO KUONA KIFURUSHI KILICHOTUPWA KWENYE PAGALA NDIPO  WALITOA TAARIFA KWA MAMA YAO, AIDHA  MAMA HUYO BAADA KUFIKA NA KUONA KIFURUSHI HICHO NI MWILI WA BINADAMU ALIPATA MASHAKA KISHA ALITOA TAARIFA KWA UONGOZI WA MTAA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
IMEONEKANA MWILI WA MAREHEMU HAUKUWA NA JERAHA LOLOTE, BALI UCHUNGUZI WA AWALI UNAOSHE KUWA WAUAJI WALIMUUA KWA KUMZIBA PUNZI KISHA KWENDA KUMTUPA  KWENYE PAGALA ENEO AMBALO SI RAHISI MTU, BASKELI AU PIKIPIKI KUPITA. PIA INAONEKANA MAREHEMU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA UGONJWA WA MATENDE KWENYE MGUU WAKE WA KUSHOTO.
POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGENE NA MAUAJI YA MWANAMKE HUYO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAPENDA KUWAELEZA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KWAMBA KAMA KUNA MTU YEYETO AMBAYE AMEPETOLEWA NA NDUGU YAKE AU JIRANI ALIYEKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI YA MATENDE AFIKE KITUO CHA POLISI, ILI AWEZE KUPELEKWA HOSPITALI YA BUGANDO ILI AWEZE KUUTAMBUA MWILI WA NDUGU YAKE, WAKATI AMBAPO JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments