Header Ads

Responsive Ads Here

STARTIMES YAZINDUA MSIMU MPYA WA KUONESHA BUNDESLIGA 2017-18 NCHINI TANZANIA


ZUHURA
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania,Ms Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa soka  wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

ZINDUA
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini. 
SHAROBARO
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu Maarufu kwa jina la Sharobora wa Kichina akielezea namna  kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Bundesliga
SALEHE
Mhariri mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga  itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali nchini.
PAMOJA
Picha ya pamoja ya waandishi wa habari na Meza Kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Ms Zuhura Hanif
PICHA NA ROBERT OKANDA
……………………………..
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog
Kampuni ya Startimes nchini Tanzania imezindua msimu mpya wa kuonesha Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kwa jina la ‘Bundeslinga wa mwaka 2017-18 ambapo mechi zote 300 zitarushwa live kupitia ving’amzi vya Startimes kupitia chanel tofauti zinazoonesha Mpira wa Miguu.
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es salaama na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wanaofatilia Mchezo wa Mpira na pia lengo kubwa ni kuwafahamisha wapenzi wa soka nchini kuanza kununua ving’amuzi na kujiunga na vifurushi hivyo kwa ajili ya kuona mechi hizo ambapo pazia la ligi hiyo litafunguliwa siku ya Ijumaa Mabingwa watetezi Bayern Munich watawakaribisha Bayern Leverkusen.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania,Ms Zuhura Hanif  amesema kuwa kuna  fursa kwa waandishi wa habari za michezo  kufanya mashindano ya  uandishi wa mechi  hizo za Ligi Kuu ya Ujerumani na mwandishi atakaeibuka mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kwenda nchini Ujerumani kushuhudia mechi na atakagharamikiwa kila kitu na Startimes.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu kwa jina la utani Sharobaro wa Kichina  amesema kuwa wana mahusiano mazuri na bundesliga  kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.
Aidha Meneja Uwendeshaji  Startimes, Gaspa Ngowi  amesema kuwa  huduma mpya ya  malipo kwa wale wenye hali ya chini  wanaweza  kulipia siku moja king’amuzi  cha Startimes  kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.

No comments