Header Ads

Responsive Ads Here

SIMBA YAANZA NA KOMBE LA NGAO YA JAMII,YAIDUNGUA YANGA5-4 KWA NJIA YA MATUTA


20953491_480647598981690_3695815636152337931_n
Timu ya Simba imetwaa Ngao ya Jamii kwa kuwafungwa watani zao wa jadi Yanga kwa hatua ya mikwanju ya Penalti  5-4 na kuchukua kombe hilo kwa mara ya tatu.

Kwa upande wa Yanga wachezaji ambao waliweza kukosa ni beki kisiki Kelvin Yondani pamoja na Juma Mahadhi huku Simba Mohamed Hussein akikosa moja ya Penalti.
Shujaa wa Simba alikuwa Mohamed Ibrahimu aliyetokea benchi alienda kumalizia Mkwanju wa mwisho ambao umepeleka Msiba kwa wanajangwani hao.
Timu zote kwa ujumla zimecheza vizuri ambapo ilipelekea dakika 90 kumalizika bila ya nyavu kunguswa na mchezaji wote hii ilikuwa mechi ya kuashiria ufunguzi wa Ligi ambayo inatarajiwa kuanza Jumamosi ya Agosti 26 na Simba watacheza na Ruvu Shooting uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Mabingwa watetezi wa Vodacom Yanga watacheza Jumapili dhidi ya Lipuli FC.

No comments