Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI YAWEKEZA ZAIDI YA EURO 37.5 KIA


muru
Na Mahmoud Ahmad Arusha Serikali imewekeza zaidi ya euro milioni 37,500,000 kwa ajili ya kukarabati miundo mbinu ya uwanja wa ndege  wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikiwa ni hatua  ya kuongeza  uwezo wa maegesho ya ndege kubwa takribani 29, kupanua  njia ya kurukia ndege na kuongeza urefu wa uwanja.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Viwanja vya Ndege  Tanzania  Bakari Murusuri amemweleza Kaitubu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga  alipotembelea na kukagua   shughuli za ukarabati wa  kiwanja hicho  jana.

Murusuri amesema mbali na ukarabati wa kiwanja pia  ametaja kazi nyingine zinazoendelea kufanyika ni pamoja na ukarabati wa  majengo ya kiwanja hicho  kuwa ya kisasa  kwa ajili ya kupokea wageni  wengi  wanje na ndani ya  nchi.

Hatua hii itakiwezesha Kiwanja  cha KIA kuhudumia  abiria  zaidi ya milioni 1.2 kwa mwaka hatua   ambayo itaongeza   idadi ya abiria kutoka idadi ya sasa ya abiria  laki 6 kwa mwaka.

Amesema kuwa ukarabati huo  umefanyika  katika mfumo wa umeme,  na kutenganisha  abiria wa ndani  na wale wa Kimataifa wanaoingia na wale wanaotoka na kazi zote hizo  zimekamilika kwa asilimia 80 hivi sasa.

Amesema  ukarabati huo unafanywa na Kampuni ya Bam  International ya uHolanzi.
 kazi hiyo inatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa Oktoba 2017 umehusisha uboreshaji wa miundo mbinu ya maji ya mvua kwa kujenga mabwawa  yanayosimamiwa na KIA yenyewe.
 
 Akizungumza mara baada ya kufanya ukazi huo Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ukarabati huo huo utaongeza idadi ya ndege kubwa  zitakazotua katika  Kiwanja hicho ambacho ni cha pili kwa ukubwa hapa Tanzania baada ya kiwanja cha Daresalaam.

Kiwanja cha ndege cha KIA kilijengwa miaka ya 1971 na miundo mbinu yake ilikuwa imechakaa na kuharibika kabisa.

Mbali na Kutembelea Kiwanja cha KIA Katibu  MKUU huyo pia ametembea Kiwanja cha Arusha  na kuelezwa kuwa  Kiwanja hicho  hivi sasa wakati wa high Season ya Utalii kinapokea ndege zaidi ya 120 kwa siku ukilinganisha na  ndege 70 wakati wa low Season.

Meneja wa Uwanda huo wa Arusha, Elinid Tesha, amesema kuwa zaidi ya abiria  18,000 wanapitia Kiwanja hicho kila siku licha ya kuwepo na changamoto ya kukosekana  kwa jengo la kisasa kwa ajili ya abiria na ofisi,ufupi wa njia  ya kurukia ndege na kusababisha ndege kubwa kushindwa kutua  uwanjani hapo.

No comments