Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI KUWAFUTIA URAIA WAKIMBIZI AMBAO HAWATAFUATA SHERIA ZA NCHI


1
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi mjini Mpanda katika mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake mkoani humo.

Mkuu wa Mkao wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga akiwahutubia wananchi wa Makazi ya Katumba,kabla ya kumkaribisha waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza katika moja ya mikutano ya Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Mwigulu nchemba.
Viongozi wa mbalimbali wakiongozwa wakfuatilia hotuba ya waziri nchemba.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Katavi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Saleh Mhando.
watanzania wapya wakimskiliza waziri wa mambo ya ndani ya nchi mwigulu nchembahayupo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mnyaki Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi 
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano huo.
…………………………………………………………………….
Serikali imeweka wazi msimamo wake  kuwa  inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi na kusisitiza vitendo vya ubaguzi  wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka  kubaguana kisiasa,kidini na kwa namna yeyote  hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.
 Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba  wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi katika  pamoja na kusisitiza kujiepusha na vitendo vya kubaguana.
 Akizungumzia kuhusu Uzalendo wa kuipenda nchi  asisitiza na kuwataka raia hao kuepukana na tabia ya za chuki dhhidi ya nchi yako badala yake uzalendouwe mbele kwanza kwa nchi. 
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga  amesema kuhusu suala la maeneo ya makzi kufutwa hati ya kuwa makazi amesema eneo hilo haliwezi kufutwa hati ya kuitwa makzi hadi hadi taratibu za kuhakikisha wale wote wanaoishi katika makazi hayo ni raia wa Tanzania na hakuna mkimbizi katika maeneo hayo lakini kama kutakuwa bado wapo wakimbizi hati haiwezi kubadilishwa hadi taratibu zikamilike.
Pia amewasisitisitiza kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.
Mapema Mkuu wa Makazi ya Mishamo na Katumba Athman Igwe alieleza kuwa kata  ya Katumba ni ya muda mrefu na ilianishwa mwaka 1972 hadi kufika sasa kuna wakazi zaidi ya 78,000 lakini asilimia tisini na saba ni ya raia wapya hivyo bado kuna wakimbizi kwenye  eneo hili.

Hivi karibuni kulikuwa na zoezi la kuhakiki wakimbizi kwa ajili ya kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu zoezi lilianza tarehe 16 mwezi wa saba na limekamilika  kwenye makazi haya mapya mwaka huu tarehe 3/8/l 2017 waliosajiliwa  waliohakikiwa ni wakimbizi 11,329  kwa kwa maana hiyo kuna kaya  5,134.
Pia Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewaasa watanzani wapya wanaoishi makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi kuondoa fikra ya kuwa wao bado wakimbizi badala yake wawe huru kwenda kuishi sehemu yeyote katika nchi maandamu wafuate taratibu na kuwasisitize wale ambao hawajachukua vyeti vyao vya uraia wachukue .
 Akihutubia  kwenye mkutano wa Hadhara katika makazi ya Katumba na Mishamo  Waziri Mwigulu ameeleza,na kuwasisitiza raia hao wapya na wale waliopatiwa vyeti vya uraia lakini hawataki kuchukua vyeti vyao waamue moja ama wachukue au waondoke kurudi kwao kwa kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuomba urai huo kama walikuwa hawautaki.
    Akizungumzia kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine katika nchi hii amesema ni jambo jema lakini amewaomba wasibadili majina yao bila kufuata utaratibu
   Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amewaasa kutunza mazingira pamoja na kusisitiza suala la kujitokeza kujiandisha kwa wale ambao hawakuandikishwa.
 Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Saidi Mselem amemweleza Waziri kuwa wananchi wa Mishamo na Katumba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali  ziazowakabili katika maeneo hayo kwa kuwa wako watanzania wapya na wale walioandikishwa.

No comments