Header Ads

Responsive Ads Here

SEKTA YA AFYA INA MAHITAJI MENGI NA MUHIMU YA KUWEKA VIPAUMBELE

NA WAMJW -ADDIS ABABA – ETHIOPIA
Mawaziri wa Afya Afrika wametakiwa kutambua kuwa Sekta ya afya ina mahitaji mengi na muhimu kwa nchi  zinazoendelea hivyo hawana budi kuwekeza kwenye vipaumbele vichache hasa vinavyohusu kuimarisha huduma za Afya ya Mama na Mtoto

 Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,  Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Mb) mbele ya Mawaziri  washiriki wa Mkutano wa 4 wa Kuondoa Vikwazo katika kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto.
“Katika mkutano huu ambao umefunguliwa na Mhe. Dkt. Mulatu Teshome, Rais wa Jamhuri ya watu wa Ethiopia unajadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kumaliza vifo vya mama na mtoto, kuongeza usawa katika upatikanaji wa huduma za Afya kwa kuondoa vikwazo, kuboresha ubora wa huduma za afya na kuimarisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango ya utoaji wa huduma za Afya” alisema Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy alieleza kwamba mipango mbalimbali na changamoto ambazo Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika zinakabiliwa nazo katika kufikia mipango endelevu ya upatikanaji wa rasimali fedha katika kutekeleza afua mbambali za sekta ya Afya.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya Rasilimalifedha  alisema Tanzania inakamilisha mchakato wa kuwa na Bima Moja ya Taifa ya Afya ambapo pia itaweka sharti kwa kila Mtu kuwa na Bima ya Afya ili kuwezesha wananchi kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapogua.
 Mbali na hayo Waziri Ummy  alisema kuwa Serikali ya Tanzania imeanzisha mikakati mbalimbali ya kuhakikisha fedha kidogo zilizopo zinatumika vizuri ikiwemo kutoa fedha kwa Vituo vya Huduma kulingana na Matokeo/utendaji wao (Result Based Financing) ambapo vituo vya tiba vilivyokuwa na hali mbaya (nyota sifuri) vinapewa fedha kuboresha huduma ambapo maboresho makubwa yameonekana katika vituo hivyo ndani ya kipindi kifupi.
Aidha Waziri Ummy alielezea uamuzi wa Serikali  wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye Vituo badala ya  kupelekwa kwenye Halmashauri (Direct Financing Facility) ambapo utekelezaji wa mpango huu umeanza tarehe 1 Julai 2017.
Waziri Ummy Mwalimu ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Muhimu wa Kimataifa wa kuondoa vikwazo katika kuokoa maisha ya Mama na mtoto unaofanyika  Addis – Ababa, Ethiopia Agosti 24 hadi 25 mwaka huu katika mjadala alioshiriki w a kuimarisha upatikanaji endelevu wa rasilimali fedha katika sekta ya afya.

No comments