Header Ads

Responsive Ads Here

RPC SHANNA-AKEMEA MADEREVA WANAOENDESHA MAGARI YAO YAKIWA MABOVU

 

IMG_20170724_124326
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna akizungumza wakati akitoa taarifa mbalimbali ya matukio yaliyotokea mkoani hapo .

Mwamvua Mwinyi
………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa rai kwa wamiliki wa magari ya abiria na binafsi  kufanya matengenezo ya magari yao pindi yanapokuwa na hitilafu ili kuepukana na ajali ambazo hugharimu maisha ya watu.
Limeeleza, madereva wasikubali kuendesha magari mabovu na wafanye ukaguzi wa kina kabla ya kuanza safari kwani ubovu wa magari huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajali.
Aidha limeweka bayana kuwa,uchunguzi uliofanyika umebaini madereva wa pikipiki maarufu bodaboda wanajali na kuthamini kukimbilia pesa zaidi kuliko kujali maisha ya watu wanaowapakia.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna,aliyasema hayo baada ya kutokea ajali mwishoni mwa wiki iliyopita Kisarawe na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 11 pamoja na ajali nyingine iliyotokea Bagamoyo ambapo gari aina ya Fuso iligongana na pikipiki uso kwa uso na kusababisha dereva wa pikipiki na abiria wake kufariki dunia.
Alisema madereva wa vyombo vya moto wamekuwa wakisababisha ajali kutokana na ubovu ,ulevi,kuwahi na wengine kuendesha wakiwa wamechoka kutokana na kuendesha safari za mbali ama usiku kucha.
Kamanda Shanna alieleza,madereva hao wanazembea kwasababu ya kulipishwa faini hivyo kuanzia sasa wataenda katika hatua nyingine ya kuwapeleka mahakamani.
‘Wanadharau wanaona kulipa faini ni rahisi,tunaenda katika hatua nyingine zaidi ya kuwafikisha mahakamani na tutaangalia namna ya mhimili huo uwanyang’anye leseni zzao wale wazembe zaidi ili iwe fundisho”alifafanua kamanda Shanna.
Kamanda Shanna alisema, wataongea na mhimili wa mahakama kuwa licha ya kutoa uhukumu pia iwanyang’anye leseni wale madereva wanaoonekana ni waembe.
Hata hivyo aliwataka madereva kijumla wabadilike ,wafuate sheria iliopo ili kuepuka  kugharimu maisha ya watu na wengine kubakia na ulemavu wa viungo.
Kamanda huyo aliwaasa madereva wa pikipiki kuwa makini wanapokuwa barabarani,ajali nyingi zinazohusisha pikipiki , wanachangia kwa kiasi kikubwa kwani wanakua na haraka ya kuwahisha wateja kwenda sehemu husika bila kuchukua tahadhari.
Akielezea ajali iliyotokea agost 13 wilayani Bagamoyo,kamanda Shanna alisema katika ajali hiyo gari iligongana na pikipiki uso kwa uso na kusababisha dereva wa pikipiki na abiria wake kufariki dunia.
Alisema,gari No.468 DJD aina na Mitsubish Fuso likitokea DSM-Bagamoyo likiendeshwa na dereva ambaye bado hajafahamika liligongana na pikipiki No.MC 315 BLM aina ya Boxer ikitokea Bagamoyo-DSM iliyokuwa ikiendeshwa na Ally Seif,miaka 19,mkazi wa Kerege wilayani hapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa pikipiki kwani ali ‘overtake’ gari lililokuwa mbele yake kwa kasi bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na gari hilo  na kusababisha vifo .
Kamanda Shanna alieleza,dereva huyo wa pikipiki na abiria wake aitwaye Mohamed Rajabu(18),mkazi wa Kerege-Bagamoyo,baada ya ajali dereva wa gari alikimbia na jitihada za kumtafuta zinaendelea.
Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya (W) Bagamoyo,gari na pikipiki vipo kituo cha Polisi Bagamoyo kwa ajili ya ukaguzi.
Jeshi hilo mkoani Pwani, linawatahadharisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali katika mkoa huo.

No comments