Header Ads

Responsive Ads Here

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA JOSSAM & CO LTD KUMALIZA BARABARA ZA KATA YA ULEDI NA ISEVYA KWA WAKATI ULIPANGWA.


Na Tiganya VincentRS –TABORA
20 August 2017
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd  kuhakikisha inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri baada ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.
Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na  Manispaa ya Tabora kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.
 Awali Mhandisi Msaidizi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Tabora Stephen  Warioba alisema kuwa ujenzi wa barabara hizo unahusisha njia za waenda kwa miguu na ipaswa inamalize katika kipindi kilichoelezwa katika Mkataba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika katika eneo husika inazingatia mambo yote yaliyomo katika Mkataba na sio nje ya hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema kuwa baada ya ujenzi wa Mradi huu kukamilika kutakuwepo na zoezi la upandaji wa miti na maua kando kando ya barabara.

No comments