Header Ads

Responsive Ads Here

PSG YAMNUNUA NEYMAR KWA REKODI YA DUNIA,KESHO KUTAMBULISHWA KWA MASHABIKI


Paris St-Germain wamekamilisha kumnunua mshambuliaji wa Brazil, Neymar, kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya ununuzi wa mchezaji ya euro 222m (£200m) kutoka Barcelona.

Ununuzi huo wa mchezaji huyo wa miaka 25 umevunja rekodi ya awali iliyowekwa Paul Pogba aliporejea Manchester United kutoka Juventus kwa £89m Agosti 2016.
Atakuwa analipwa euro 45m (£40.7m) kwa mwaka – euro 865,000 (£782,000) kila wiki – kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya £400m.
Neymar amesema amejiunga na “mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi Ulaya”.
“Ndoto kuu ya Paris St-Germain ilinivutia kujiunga na klabu hiyo, pamoja na kujitoleza kwao na nguvu zinazotokana na hili,” amesema.
“Najihisi niko tayari kuanza kazi. Kuanzia leo, nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya.”
Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa imepanga kuwa na kikao na wanahabari mwendo wa saa 12:30 BST Ijumaa (saa nane unusu Afrika Mashariki).
Neymar baadaye atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG Jumamosi wakati wa mechi yao ya kwanza kabisa ya msimu mpya, ambayo itakuwa nyumbani uwanja wa Parc des Princes dhidi ya Amiens.

No comments