Header Ads

Responsive Ads Here

PROFESA MBARAWA AHIMIZA KASI YA UJENZI UBUNGO INTERCHANGE.1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akizungumza na Mkandarasi wa China Civil Engeneering Construction Corporation (CCECC), anayejenga barabara za juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange), Jijini Dar es Salaam.

2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia) akikagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma (ubungo interchange) jijini Dar  es Salaam.
3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akielekeza jambo kwa Mkandarasi wa China Civil Engeneering Construction Corporation (CCECC), anayejenga barabara za (Ubungo Interchange), alipokagua vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huo.
4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa (Ubungo Interchange), alipokagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo, Jijini Dara es Salaam.
5
Msimamizi wa ujenzi wa (Ubungo  Interchange) eng. Hendrish Nyange akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) kuhusua hatua za awali za ujenzi wa barabara hizo wakati Waziri alipokagua maandalizi ya Ujenzi huo.
……………………….
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Dar es Salaam , Uongozi wa Manispaa ya Ubungo na Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT), kushirikiana ili kuondoa vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi anayejenga barabara za juu katika makutano ya ubungo (interchange).
Akizungumza mara baada ya kukagua kazi za ujenzi zinazoendelea katika mradi huo Profesa Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wadau hao kushirikiana ili kuwezesha eneo la ujenzi kuwa safi na salama wakati wote na hivyo kuongeza kasi ya ujenzi.
“Hakikisha mifumo ya umeme, maji, mawasiliano ya simu na gesi iliyopita katika eneo la mradi huo inaondolewa haraka na kwa usalama bila kuathiri huduma kwa wananchi”, amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amekagua maabara ya kuchunguza udongo, ujenzi wa nguzo za barabara za juu, mtambo wa kutengeneza zege na barabara zitakazotumika wakati ujenzi ukiendelea na kuzungumzia umuhimu wanafunzi wengi wa mafunzo kwa vitendo kupewa fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi ili kuongeza wataalam wazalendo.
Aidha Profesa Mbarawa ameutaka uongozi wa Manispaa ya Ubungo kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo (machinga), katika eneo hilo ili kupisha kazi za ujenzi.
Naye Meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa vikwazo vyote katika eneo la mradi vitaondolewa ikiwemo majengo yaliyopo ndani ya eneo la mradi katika kipindi kifupi.
Kiasi cha shilingi bilioni 177 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo zinazojengwa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation kwa miezi thelathini na kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dare s salaam.
Imotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments