Header Ads

Responsive Ads Here

NGO’S TUMIENI FURSA HII KUHAKIKI NA KUSAJILI NGO’S ZISIZOSAJILIWA: SIHABA NKINGA


Pix 1
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Asasi za Kirai nchini na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma katika uzinduzi wa uhakiki wa Asasi za Kiraia Agosti 21,2017.

Pix 2
Msajili wa Asasi zisizokuwa za kirai Bw. Marcel Katemba akisisitiza jambo kuhusu mwitikio chanya uliooneshwa na mashirika hayo katika uandaaji wa uhakiki wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali katika kikao na waandishi wa habari mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Pix 3
Mwenyekiti wa Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Nicholous Zakaria akipongeza azma ya Seriklai kuendesha uhakiki wa mashirika yasiyokuwa ya kireikali katika kikao cha uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Dodoma Agosti 21,2017.  
Pix 4
Mwenyekiti wa Maandalizi ya Uhakikiki wa Asasi zisizokuwa za Kiserikali Bw. Onesmo Olenguruma akielezea kuridhishwa na ushirikishwaji wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiseriklai katika kuendesha uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini Agosti 21,2017.
Pix 5
Katibu Mkuu Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Ismail Suleiman akisisitiza kuendeleza mashirikiano katika kufanikisha uhakiki wa mashirika yasiyoya kiserikali ambao katika kiako cha uzinduzi kilichofanyika mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Pix 6 c
Baadhi ya wadau kutoka Asasi za Kirai nchini, watendaji wa Wizara na waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa uhakiki wa mashirika yasiyo ya kiserikali uliozinduliwa mkoa Dodoma Agosti 21,2017.
Pix 7
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa asasai zisizo za kiserikali muda mfupi baada ya uzinduzi wa kazi ya uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini Agosti 21,2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW


 ………………………………

Na Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amewashauri wamiliki wa Asasi za kiraia (NGOs) kutumia fursa ya muda uliotolewa na Wizara kuhakiki asasi zao na wale ambao hawajasajili asasi zao kuzisajili.
Ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizindua mpango wa kuhakiki Asasi zisizo za kiraia unaoanza Agosti 21, 2017 na kumalizika Septemba 4, 2017.
Ameongeza kuwa suala la kuhakiki Asasi za kirai ni la muhimu na litapelekea kupata kubaini asasi hizo nchini na mchango wao kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Niyaombe yale mashirika ambayo yanafanya kazi za NGO’S na hayakusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya NGOs yatumie fursa hii kujisalimisha na kujisajili’’ alisema Bibi Sihaba.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Nicholous Zakaria ameishukuru Serikali kwa kuchukua hatua nzuri ya kuhakiki Asasi hizo ili kupata taarifa zilizo sahihi kuhusu asasi hizo kwa maendeleo ya asasi, jamii na taifa kwa ujumla.
“Nichukue fursa hii kuipongeza Serikali kwa ushirikiano mnaotupatia kupitia Waziri,  Katibu Mkuu na Msajili wa Asasi za kiraia katika kufanikisha shughuli zetu za kila siku” alisema Bw. Nicholous Zakaria.
Katika kuhakikisha zoezi la uhakiki linafanikiwa na kuwafikia wadau wengi zaidi Wizara imegawa uhakiki katika Kanda tano ambazo ni Kanda ya Mashariki itakayohudumia mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Morogoro na Pwani, Kanda ya Kati itakayohudumia mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida, na Dodoma, kanda ya Ziwa itakayohudumia mikoa ya Geita, Shinyanga, Mara, Kagera na Mwanza, Kanda ya kasikazini itakayohudumia mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, Kanda ya Nyanda za Juu itahudumia mikoa ya  Katavi, Rukwa, Ruvuma, Njombe, iringa na Mbeya.
Aidha, mmiliki wa asasi anaweza kupata huduma ya usajili katika kituo kitakachokuwa karibu ili kufanikisha zoeezi la uhakiki ambalo litatoa sura halisi ya idadi, shughuli na mchango wa kisekta katika maendeleo ya Taifa.

No comments