Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI AKUTANA NA WATENDAJI WA TANESCO –MTWARA


Picha Na 1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara

Picha Na 2
Sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Picha Na 3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo akisisitiza jambo katika kikao hicho
Picha Na 4
Afisa Rasilimaliwatu wa Kanda ya Kusini, Bonus Msuha (kushoto) akieleza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Meneja wa TANESCO-Mtwara Mhandisi  Aziz Salum
Picha Na 5
Sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara na Wizara ya Nishati na Madini  wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
……………………….
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo leo tarehe 24 Agosti, 2017 amefanya kikao cha kazi na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za utendaji kazi. Dkt. Pallangyo amewataka watendaji hao  kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwasilisha  taarifa za utekelezaji za kila baada ya miezi mitatu.

No comments