Header Ads

Responsive Ads Here

MWENYE TATIZO LA MTINDIO WA UBONGO AISHI MIAKA MITANO KWA KUFUNGWA KAMBA MIGUUNI.


Binti Lyaki Juma akiwa amefungwa na kamba miguuni kwake ili hastoroke Nyumbani kwao.

Lyaki Juma akiwa kwenye mazingira ya nyumbani kwao.   

Msichana mwenye umri wa miaka 26 mkazi
wa mtaa wa nyakato Kata ya Ihanamilo kwenye Halmashauri ya mji wa Geita
anadaiwa kufungwa kamba kwenye miguu yake kwa zaidi ya miaka mitano kutokana na
tatizo la mtindio wa ubongo.
Msichana huyo anayejulikana kwa
Jina la Lyaki Juma ambaye anaishi kwa kufungwa kamba miguuni kwa madai kuwa amekuwa
akitoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana hali inayompa wakati mgumu mama
yake mzazi kwa kumtafuta licha ya hatari anazokutana nazo ikiwemo kubakwa na
watu wenye nia ovu.
Mama Mzazi wa Msichana huyo Mwakami
Shingashinga amezungumza  na Maduka
online  ambapo  amesema mwanaye alimzaa akiwa na akili timamu
lakini alianza kubadilika alipofikisha umri miaka saba baada ya kuanza
kuugua mara kwa mara.
 “Mwanangu alianza kupata
tatizo hili baada ya kufikisha miaka saba alikuwa akikimbia na kwenda kusikojulikana
na hata nilipomtafuta nilikuwa nikimkuta yupo mbali na eneo la nyumbani muda
mwingine namkuta mlimani”Alisema Mwakami.
  Jirani wa karibu wa
Familia hiyo Bi Verediana Joseph amesema kuwa mama huyo ana shida kutokana na kutokuwa
na uwezo wa kumhudumia mtoto huyo kwani kipato chake cha kifedha ni kidogo.
“Kiukweli hali ya mama huyu
inasikitisha sana kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha na hata hivyo kuna
watu ambao hawana nia nzuri wamekuwa wakimbaka na kumfanyia kitendo cha kinyama
binti yake pindi anapokuwa ametoka kikazi hivyo naweza kusema kuwa amekuwa
akiishi kwa wasiwasi sana na muda mwingine anakosa amani kutokana na watu
kushindwa kumuhurumia”Alisema Bi,Verediana.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato
Charles Kulola ameelezea kuwa mtoto huyo ana baba yake Mzazi lakini amekuwa
akimkana kuwa sio mwanawe.
“Baba yake anaitwa Juma yupo
kabisa hapo mtaa jirani lakini jambo la kusikitisha ameendelea kumkana mtoto
wake jambo ambalo sisi tunaona kuwa sio zuri kwani ukizaa mtoto mlemavu kuna
sababu gani ya kumkataa jamani mbona watu wanakosa imani”Alisema Mwenyekiti.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

No comments