Header Ads

Responsive Ads Here

Muungano wa Nasa Watishia Kutoyatambua Matokeo ya Uchaguzi Nchini KenyaWakati matokeo ya uchaguzi Mkuu nchini KENYA yakiendelea kutolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini humo IEBC, viongozi wa juu wa muungano wa vyama vya upinzani NASA usiku wa kuamkia leo wamepinga matokeo hayo wakidai ni batili na hayaendani kabisa na yale ambayo yamesainiwa kwenye fomu namba tatu ya iliyosainiwa na mawakala wa kwenye vituo.


MUSALIA MUDAVADI ni miongoni mwa viongoz wa juu wa NASA ambaye usiku wa kuamkia leo amefika kwenye kituo kikuu cha kukusanya na kutangaza matokeo hayo jijini NAIROBI kuelezea Dhamira ya Nasa Kukataa Matokeo Hayo
Kauli ya MUDAVADI ikaungwa mkonona msemaji muu wa Umoja huo JAMES ORENGO ambaye amesema mfumo unaotumika kuhesababu matokeo hayo ni batili.
Hadi sasa bado matokeo yanaendelea kutangazwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC mbao katika nafasi ya urais mchuano mkali umeendelea kuwa baina ya viongozi wawiili UHURU KENYATA wa JUBILEE na RAILA ODINDA ambao wanapishana kwa kura chache.
Hadi asubuhi hii UHURU KENYATA alikuwa na zaidi ya kura milioni 6.5 huku ODINGA akimfuatia kwa kura zaidi ya milioni 5.4.

No comments