Header Ads

Responsive Ads Here

MONDULI INAKABILIWA NA ONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI


pic+fursa+za+kujiendeleza
Na Mahmoud Ahmad Monduli

Wilaya ya monduli bado inakabiliwa na changamoto kubwa la ongezeko la mimba za utotoni ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wanafuzni 45 shule za msingi walipata ujauzito na 33 wa shule za sekondari kuanzia mwaka 2015 hadi july 2017 ambapo wanafunzi hao wameacha shule kutokana na hali hiyo ambapo imewarudhisha nyumba katika kupambana na adui ujinga.

Hayo yameelezwa leo na Afisa elimu sekondari Rebeca Mbaga wakati akiwasilisha taarifa fupi katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na mimba za utotoni iliyofanyika katika wilaya ya monduli ambapo ilihusisha wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo wanafunzi wa shule zamsingi na sekondari kutoka wilayani hapo ,mkoa wa arusha.
Hata hivyo alisema kuwa lengo hasa la kuzindua kampeni hiyo nikutaka kuangalia namna ya kuzuia tatizo hilo lisiendelee na kuchukua hatua kali kwa wale wotye wanajihusisha na mapenzi na watoto washule na kuwadanganya na kuwakatiza ndoto na masomo yao.
Aidha aliongeza kuwa takwimu hizo nikubwa ukilinganisha nakipindi kifupi cha watoto hao kukaa mashuleni hata hivyo amewataka wadau kuwa walizni na kuwasaidia kuwabaini wale waliofanya vitendo hivyo viovi ambavyo vinaenda kinyume na jitihada za Rais kuweza kutoa elimu bure na kupambana na wale wote wanaowaghilibu wanafunzi na hata kuwakatisha masomo yao hatua kali zichukuliwe dhizi yao ili iwe fundisho kwa jamii na familia za watoto.
 Kwa upande wake Mratibu wa huduma za afya na uzazi kutoka hospitali ya wilaya ya monduli Rachel kivumba alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2016 kati 8537 kati yao 1936 ambao wako chini ya miaka 20 walipata ujauzito na mwaka 2017 kati ya 3875 kati yao 851 ambao wako chuini ya miaka 20 walipata ujauzito na kujifungua mbapo limekuwa tatizo kubwa ambalo linapotyeza nguvu kazi ya taifa na ndoto za watoto hawa.
Ambapo madhara yatokanayo na kubeba ujauzito mapema ni kutokomaa kilakili kwa watoto hawa na nyonga zao na mifupa haijakomaa kuweza kuhimili uzito wa mtoto kukua akiwa tumboni hali ambayo wengine wanalazimika kufanyiwa upasuaji na baadhi yao kutokwa na damu nyimgi hata kupelekea kupoteza maisha yao.
Kwa upande wake Afisa ustawi wajamii Monduli Denis Mgie alisema kuwa miongozo na kanuni na sheria za mtoto zinakinzana kama sheria no 21 ya mtoto ya mwaka 2009  katika kupata haki yake ya kimsingi kwani inatofautina katika tafsiri ya mtoto kuna haja ya kuweza kurekebisha upya ili kumwezesha mtoto kupata haki yake.
Kwa upande wake Mkuu wa dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la polisi Monduli Regina Wilbert alisema kuwa wanapokea kesi nyingi sana  ambapo mwaka 2016 zlilipotiwa kesi 45 ambapo kati ya hizo kesi 28 zilihusisha wanafunzi wa shule za msingi  ambapo mwaka 2016 kesi 7 tu zilienda mahakamani na mwaka 2017 kesi zilizoripotiwa nikesi 29 na kati ya hizo kesi 12 tu zilihusisha wanafunzi wa msingi na kesi 9 zilihusisha wanafunzi wa sekondari kati ya hizo kesi 4 tu zilienda mahakamani.
Ambapo ukilinganisha kesi wanazopokea na kupelekwa mahakamani bado kunakuwepo na changamoto nyingi katika jamii kuweza kukamilisha vielezo vya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani ikiwemo mila potofu ambapo zinakuwa nichangamoto katika kutoa ushahidi  ,kuogopa laana kuotka kwa wazazi kutowataja waliohusika kuwapa mimba ,uelewa mdogo wa kutunza vielelezo vya udhalilishaji pamoja mna mhanga kudhalilishwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Monduli Julius Kalanga kupitia chama cha demokrasia (CHADEMA)alisema kuwa Serikali izingatie dhana ya ushirikishwaji bila ya kujali tofauti zilizoko katika kutafuta ufumbuzi wasuala hili la mimba za utotoni kuweza kumaliza tatizo hili amballo linaonekana kuonekana linaongeza katika wilaya hiyo.
Aliwataka wazazi kuwa makini katika kuwalinda watoto wao na kushirikiana na walimu kuweza kuhakikisha watoto wanapata elimu yao ya msingi hadi chuo kwa wakati na bila ya kuwa na vikwazo vyovyote vinavyoweza kuwakwamisha kufikia ndoto zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wahalmshauri ya wilaya ya monduli Issack Joseph kupitia chama cha chadema alisema kuwa alisema kuwa wanasimamia kauli ya Rais wa nchi ya kuwa mwanafunzi yeyote atakae pata miba hataruhusiwa kuendelea na masomo hivyo basi amewataka wanafuzni kuweza kusimamia masomo yao na waweze kujitambua kwa kusoma tu na sio kuchanganya mambo mengine ambayo wakati wake bado .
Na amewataka wanafuzni hao endapo mtu yeyote atawalazimisha kufanya kitu kinyume na utaratibu washitaki kwa uongzi husika ili kuweza kufanyiwa kazi ili kuweza kuwasaidia watoto hao kupata haki yao ya msingi ya elimu kwani ndio nguzo ya maisha ya mtoto yeyote mwenye sifa za kupata elimu.
mwisho..
kutoka kwa jamii ambazo wanakuja kushataki lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo 

No comments