Header Ads

Responsive Ads Here

MKUU WA MKOA WA LINDI AHIMIZA MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI


DSC_0443
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambiakipewa Maelezo na Afisa Vipimo juu ya Mizani ya iliyoundwa na Watanzania.

DSC_0448
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambiakitoamaagizo  kwa Wakala wa Vipimo kusimamia matumizi ya vipimo sahihi katika msimu wa ununuzi wa mazao.
DSC_0456
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godyfrey W. Zambiakisaini Kitabu cha wageni katika Maonesho ya Nanenane.
……………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambiamewataka Wakala wa Vipimo Kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia matumizi sahihi ya vipimo katika maeneo mbalimbali,  ili wakulima na Wananchi kwa ujumlawaweze kunufaika na mazao wanayolimapindiwaendapokuyauza wakati wa msimu.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo alipotembelea banda la WMA, katika maonesho ya nane nane ambayo kitaifayanafanyika katika mkoa wa Lindi kwenye viwanja vya ngongo.  Pia amewataka Wakala wa Vipimo kushirikiana na maafisa waliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa katika kuhakikisha wakulima hawapunjwipindiwaendapo kuuza mazao yao. kwani baadhi ya wafanyabiashara  wasio waaminifu, huchezea mizani yao kwa lengo la kuwapunja wakulima kwa lengo la kupata faida zaidi.
Vilevile Mhe. GodyfreyZambialielezwana maafisa wa vipimo namna kangomba inavyowapunja wakulima, kwa kuwa siyo kipimo sahihi kinachopaswa kutumika kununulia mazao.  Hivyo Wakala wa Vipimo inawapa wakulima elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyohakikiwa.  Pia wanaelekezwa namna ya kutambua alama zinazowekwa kwenye vipimo vilivyohakikiwana Wakala ambazo ni  stika maalum, pamoja nakugongwanembo ya Taifa na tarakimu mbili za mwisho za mwaka husika. Mfano kwa mwakahuu 2017,itasomeka namba 17.
Akizungumzanamwandishi wetu baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Afisa Vipimo wa Lindi Bw. NyagabonaMkanjabiamesema,wamejipanga vizuri katika kusimamia matumizi ya vipimo sahihi na kuhakikisha mizani zote zinazotumika katika vyama vya ushirika vya msingizinakaguliwa kabla ya misimu ya kuuza mazao kuanza. Pia watahakikishakaguzi mbalimbali za kustukizazinafanyikakipindi cha msimu wa kuuza mazao unapofika.
Pia, amewakaribisha viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi pamoja na wananchi wote kutembelea banda la wakala wa vipimo katika maonesho ya nanenane mkoa wa Lindi na kujionea Mizani mbalimbali zinazopaswa kutumika katika ununuzi wa bidhaa mbali mbali na mazao ukiwemo mzani wa digital wa tani 2 ambao unapima bidhaa/mazao na kutoa risiti hapo hapo
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa waLindi Bw. Andrew Mbwambo ametoawito kwa Wakulima, wafanyabiashara na Wananchi wote kutojihusisha na vitendo vya kuchezea vipimo kwani kwa sasa adhabu ni kubwa baada ya Sheria ya Vipimo Sura namba 340 na Mapitio yake ya mwaka 2002 kufanyiwa marekebisho mwaka 2016.

No comments