Header Ads

Responsive Ads Here

Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kutafsiriwa kwa Kiswahili


Pix 00
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi akifungua mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Pix 00A
Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Anna Maembe akifafanua jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 01
ka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi. Maimuna Tarishi (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula, wakiendelea na mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo jijini Dar es Salaam.
Pix 03
Baadhi ya wadau wa kutetea haki za wanawake na watoto wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Anna Maembe wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 03b
Baadhi ya wadau wa kutetea haki za wanawake na watoto wakiendelea na mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Pix 05
Mkurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene akitoa mada wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
…………………………..
Na: Anthony Ishengoma,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto inatafsiri kwa Kiswahili Mkakati wa Taifa wa miaka mitano wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ili kurahisisha mawasiliano kwa kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kijiji.
Hayo yamebainika Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Sihaba Nkinga, wakati wa Kikao kazi na wadau wa Maendeleo kuchangia fedha za utekelezaji wa Mkakati huo.
Mkakati huo unatafsiriwa ili kutatua changamoto ya mawasiliano iliyopo katika utekelezaji wake kuanzia ngazi za chini hadi juu Kitaifa ili kurahisisha utekelezaji wake ikiwa ni namna mojawapo ya kuimarisha na kutafuta namna bora ya kurahisisha mawasiliano katika ngazi zote.
Mkutano huo na wadau wa maendeleo unalenga kutafuta fedha takribani Tsh. bilioni 250 za Tanzania zitakazo tolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo ili kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huo Nchini kote.  
Wakati huohuo Katibu Mkuu  Ofisi ya Wiziri Mkuu  Maimuna Tarishi wakati wa kutoa salamu za ufunguzi wa kikao kazi hicho amesema mchakato wa utengenezaji wa Mkakati huo ulizingatia sana malengo ya millennia ya 2030 na Malengo ya Agenda 2063 ya Tume ya Umoja wa Afrika na kusisitiza kuwa kinachotakiwa sasa ni kutafuta namna bora ya utekelezaji wa Mkakati huo.
Tanzania ni moja ya Nchi nne  Duniani na ya kwanza Afrika kupewa nafasi ya mfano kuwa katika nafasi nzuri ya kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kwa sababu ya mchango wake katika tafiti zinazohusiahana na masuala ya ukatili.

No comments