Header Ads

Responsive Ads Here

MBAO FC YAZIDI KUIMARIKA,YAPATA UDHAMINI WA MAMILIONI KUTOKA GF TRUCK $ EQUIPMENT


Kampuni ya GF Trucks $ Equipment Ltd imetoa udhamini wa shilingi milioni 140 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala alisema udhamini huo utaendana na kuwapa basi la kusafiria lenye thamani ya shilingi milioni 70.
Bundala alisema, huo ndiyo mwanzo wa kuidhamini Mbao huku akiahidi mambo mengine mazuri zaidi.
 
Alisema kuwa, wamefikia hatua ya kuidhamini hiyo kwa ajili ya kujitangaza zaidi kupitia Mbao ambao walifanya vema kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
 
 
“Jumla ya udhamini tulioutoa wa shilingi milioni 140 kati ya hizo milioni 70 zimetumika kuwanunulia basi la kusafiria na milioni 70 nyingine wamewapa kwa ajili ya matumizi mengine binafsi yatakayoendelesha timu yao, “alisema Bundala.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao, Solly Nyashi alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa udhamini walioutoa kwa timu yao.
“Niwashukuru kampuni ya GF Truck $Equipment Ltd kwa udhamini huo waliotupa kiukweli kabisa kama mnavyofahamu Mbao timu inasafiri  hivyo tunaamini hili basi walilotupatia linatosha kabisa kuturahisishia safari zetu, “alisema Nyashi.

No comments