Header Ads

Responsive Ads Here

MANISPAA MPYA YA UBUNGO YAFANIKIWA KUNUNUA MAGARI MATANO YATAKAYOTUMIKA KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO


A
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri mpya ya Manispaa ya Ubungo akizungumza na baadhi ya watumishi pamoja na madereva hawapo pichani mara baada kufanyika kwa halfa fupIi ya kumkabidhi magari matano ambayo yamenunuliwa na manispaa  hiyo kutokana na fedha za mapato ya ndani

D
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri mpya ya manispaa ya Ubungo akizungumza jambo la baadhi ya madereva na watendaji hawapo pichani mara baada ya halfa fupi ya kukabidhi maari matano ambayo yamenunuliwa na manispaa hiyo kutokana fedha zake za makusanyo ya ndani kwa lengo la kuweza kuboresha ukusanyaji wa mapato
PICHA NA VICTOR MASANGU.
……………………..
NA VICTOR  MASANGU, KIBAMBA
HALMASHAURI mpya ya manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam katika kuhakikisha inamuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk.John Magufuli katika kuboresha ukusanyaji wa kodi imefanikiwa  kununua magari matano mapya ambayo yatapelekwa  katika kata tano kwa ajili ya kuongeza ufanisi zaidi  katika suala zima la mapato pamoja na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Akizungumza kati halfa maalumu  iliyoandaliwa kwa ajili ya kuweza kuwakabidhi madareva magari hayo matano imefanyika  katika Ofisi hizo  zilizopo maeneo ya kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Kayombo amebainisha kuwa  magari hayo yamenunuliwa kutokana na makusanyo ya fedha za ndani.
Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza  kuwa magari hayo wameamua kuyapeleka yote katika idara ya fedha na biashara kwa lengo la kuweza kutimiza azma ya serikali ya kuongeza makusanyo ya kodi pamoja na kuweza kuwapa fursa watendaji  wote kuweza kutekeleza na kusimamia ipasavyo  majukumu yao ikiwemo sambamba  na kuwatumikia wananchi.
“Kwanza kabisa napenda kuwashukuru na kuwapongeza watendaji wote wa halmashauri mpya ya ubungo pamoja na madiwani kwa kuweza kujituma kwa hali na mali hadi tumefikia hatua hii, maana gari hizi tumenunua kupitia vyanzo vyetu vya ndani vya mapato kwa hiyo hii ni hatua kubwa na itaweza kutimiza malengo ambayo tumejiwekea katika kuleta maendeleo na kukusanya mapato,”alisema Kayombo.
Kayombo aliongeza kuwa lengo lao kubwa la kununua magari hayo matano ni kwa ajili ya kuweza kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa watendaji kuweza kufika katika maeneo mbali mbali ili kukusanya kodi na kuongeza mapato ya ndani ambayo yataweza kusaidia katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.
Awali Mkurugenzi huyo kabla ya kuyakabidhi rasmi magari hayo akusita kuwaasa madereva hao kuachana na tabia ya kuyatumia magari hayo kwa shughuli zao binafsi na kupiga marufuku vitendo vya kuyapaki katika sehemu za starehe hasa katika nyakati za usiku kwani yamenunuliwa kutokana na fedha za wananchi wenyewe.
Kwa upande wake Mweka hazina wa manispaa hiyo ya Ubungo  Jane Machicho  pamoja na Mhasibu wake Paulo Kandukandu walisema kwamba kununuliwa kwa magari hayo matano waliyoyapata kwa kipindi cha miezi nane   kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na kwamba kwa mwaka huu wa fedha  wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 23.
Nao baadhi ya madereva wapya waliokabidhiwa magari  hayo akiwemo Lucian Peter pamoja na Abdalah Mfinanga wamemwakikishia mkurugenzi k kuyatunza magari hayo  na kuzingatia maagizo ambayo ameyatoa licha ya wakati mwingine wanakabiliwa na changamoto mbali mbali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila.
MAGARI hayo matano ambayo yamenunuliwa na halmashauri mpya ya manispaa ya ubungo kwa kipindi cha miezi minane  kutokana na fedha zilizotokana na  mapato ya ndani ambapo gari hizo zitagawanywa katika kata tano za Manzese,Ubungo,Sinza, kwembe pamoja na kata ya Kimara kwa kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato na miradi mingine ya maendeleo.

No comments