Header Ads

Responsive Ads Here

MAKONDA ALIONGEZEA NGUVU SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC


NOA1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhi msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania  TBC  Bi. MARTHA SWAI .

NOA2
Hizi ni Pikipiki tatu zilizokabidhiwa kwa TBC ikiwa ni miongozi mwa vifaa vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa huyo kwa Shirika hilo.
………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametoa msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.
Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia Makonda amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la TBC kuanzia siku ya kesho ili liwe na mwonekano wa kisasa.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo MAKONDA amesema lengo ni kuwawezesha Wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.
Makonda ametoa msaada huo baada ya kufika Ofisi za TBC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa ikiwemo Usafiri, Camera na Computer ambapo kwa sasa Gari na Pikipiki hizo zitawawezesha Waandishi kufika kwenye matukio kwa uharaka huku*Compute* zikimuwezesha  Mhariri kutekeleza majukumu yake.
Vifaa hivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBC * Bi. MARTHA SWAI amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo kuku Zaitun Mkwama ambae ni mtayarishaji wa kipindi cha Hadubini akieleza kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao.

No comments