Header Ads

Responsive Ads Here

Madiwani kutokuwa wachezaji wakati huohuo marefarii


MAGAMadiwani wametakiwa kutokuwa vikwazo na kusababisha ubadhirifu wa fedha za wananchi kwa kujipa zabuni ya miradi katika Halmashuri wanazoziongoza kwani mara nyingi hali hiyo imekuwa chanzo cha migogoro na mvurugano unaokwamisha maendeleo kwa wananchi.

Hayo yamesemwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. Emmanuel Maganga wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri Wilaya ya Kasulu. Ameqaeleza kuwa sasa tuondoe dhana ya kwamba nyadhifa zetu za kisiasa zitumike kukamata zabuni za Halmashauri “pengine tumetumia rasilimali nyingi kutafuta nafasi hizi za kisiasa ili tuje tupate faida kwa kuchukua tenda za Halmashauri basi nawaomba tutoke katika katika ulimwengu huo wa zama za kale”.
Aliongeza kuwa yeye anawaunga mkono madiwani pale wanapothibitisha Mtumishi au mtendaji amefanya ubadhirifu wamchukulie hatua lakini si kama ilivyozoeleka siku za nyuma Mtumishi anapotumia utaalam wake wa kitaaluma basi anaonekana mkwamishaji wa mipango ya wizi dhidi ya baadhi ya madiwani “hili halikubaliki, tuwaache wataalam wafanye kazi zao sisi tuwasimmie tu” aliongeza Maganga.
Aidha ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ameipongeza kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Amewaomba waheshimiwa Madiwaninkujisomea Sheria mbalombali za uendeshaji wa wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutokuwa na mkanganyiko na mwingiliano wa utendaji katika maeneo yao.
Mara nyingi tumekuwa tukiwaadhimiwa watendaji kwa makosa ya kutokubaliana na haja zetu binafsi badala ya kuangalia maslahi mapana ya Umma. Nawaomba tuchape kazi kwa maslahi ya wananchi amezidi kuwasisitiza.

No comments