Header Ads

Responsive Ads Here

MABINGWA WATETEZI WA VPL WAANZA NA SARE,YABANWA MBAVU NA VIJANA WA MATOLA


DSC_0370
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga SC imeanza msimu kwa sare ya kufungana goli 1-1 na Lipuli FC ya Iringa timu ambayo imepanda daraja msimu huu ikiwa inafundishwa na kocha Selemani Matola mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru ‘Shamba la Bibi’ jijini Dar es salaam.

Lipuli ilianza kupata  dakika ya 44 baada ya Seif Abdallah kuachia shuti kali lililomshinda golikipa wa Yanga Youthi Rostand kisha mpira kujaa wavuni baada ya kuwachachafifya mabeki wa Yanga upande wa Gadier Mbaga.
Yanga walisawazisha bao  dakika ya 45 goli ambalo limefungwa na Donald Ngoma aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Juma Abdul.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayakuweza kusaidia timu zote kuweza kuondoka na pointi tatu na dakika za lala salama Lipuli walipata pigo baada ya beki wao Kwansi Asante kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu.

No comments