Header Ads

Responsive Ads Here

MAAMBUKIZI YA MALARIA YAPUNGUA TANZANIA


2
 Kiongozi Uchunguzi na Matibabu ya Malaria Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt. Sigsbert Mkude akielezea Mikoa yenye maambukizi ya malaria nchini wakati wa semina ya siku moja kuhusina na hali ya malaria Nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2017

  5
Moja ya kipimo cha utafiti kikionyesha maambukizi ya Maralia Kanda ya Magharibi kati ya  mwaka 2016 na 2012
6
Baadhi ya waandishi wakifuatilia mada katika semina hiyo.3
7
 Mwalimu wa Kitengo cha Udhibiti Mbu waenezao Malaria kutoka Wizara ya Afya, Dkt, Charles Dismas akielezea mada kuhusina na maambukizi ya Malaria.
……………………………………………………………….
 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema hali ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria imepungua kutoka asilimia 90 ya maeneo yenye mbu  hadi kufikia  asilimia 50  ya walioambukizwa  malaria tangu 2000 hadi 2017.
Hayo yamebainishwa  na Dkt. Sigsbert Mkude,  Kiongozi Uchunguzi na Matibabu ya Malaria nchini Tanzania , (NMCP) alipokutana na Waandishi wa Habari Ukumbi wa Luther House leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt, Mkude amesema; “Kwa miaka 15 sasa viwango vya maambukizi ya malaria vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50,. Aidha,  idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria vimepungua kwa asilimia .0,  ikilinganishwa na miaka ya nyuma”
Ameongeza kwa kusema; “Mikoa ya Kaskazini ndiyo inayoongoza kwa idadi ndogo ya wagonjwa  na maambukizi ya ugonjwa wa malaria hapa nchini, amesema Dkt Mkude 
Akitoa takwimu hizo Dkt. Mkude amebainisha kuwa, mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Kagera na Geita  na mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambayo ni Mtwara na Lindi ndiyo inayoongoza kwa maambukizi pamoja na idadi ya vifo kwa zaidi ya asilimia 50 toka mwaka 2008 hadi 2016.
Akieleza sababu za kiwango hicho kuongezeka amesema; “Tofauti ya kijiografia ndiyo zinazochangia maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu kati ya mkoa mmoja na mwingine. Kwani Mbu wana tabia ya kustahimili kuishi na kuzaliana kwenye maeneo yenye joto kuliko maeneo yenye baridi kali,”
Aidha Dkt. Mkude alifafanua kuwa idadi kubwa ya watu wanaoambukizwa  ugonjwa wa malaria ni wenye kipato cha chini na waishio vijijini. Ambapo, ni zaidi  ya asilimia 90 wanaokaai kwenye maeneo yenye maambukizi ya Malaria hapa nchini.
Naye Dkt,  Charles Mwalimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Mbu-Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria amesema ; Serikali imefanya mikakati ya kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kugawa vyandarua vyenye viuatilifu, kupulizia dawa katika makazi ya watu, kutunza mazingira kote nchini  na kupulizia viuatilifu katika maji yaliyotuama katika baadhi ya maeneo Kanda ya.Ziwa
“Mikakati huu umesaidia kuinua mwitiko wa watu kutumia vyandarua pamoja na kutunza mazingira na umeleta matunda ya uthibiti wa ugonjwa kwa jamii ya watanzania wengi,” alifafanua Dkt. Mwalimu.
Aidha, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, unakumbana na  changamoto kadha ambazo imani potofu katika matumizi ya vyandarua  ambazo tunapambana nazo ili kumaliza  tatizo la malaria hapa nchini. amesema Dkt Mwalimu.
Vilevile kuna changamoto ya vyandarua kufugia kuku, kuweka uzio kwenye bustani, kuvulia samaki katika maeneo ya wavuvi, hususan Kanda ya Ziwa, na imani kuwa matumizi ya vyandarua hivyo hupunguza nguvu za kiume na kusababisha vifo vya watoto wadogo. Ameifafanua Dkt. Mwalimu.
Wizara imefanyia kazi changamoto hizo na inaendelea kuhamasisha  umma juu ya  ufahamu wa ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria. Elimu inatolewa juu ya matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu, kuhifadhi mazingira pamoja na kuijengea uwezo, kuiwezesha na kuisaidia mikoa na halmashauri ili, kupambana na malaria hapa nchini.

No comments