Header Ads

Responsive Ads Here

LUKUVI AWATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU MATAPELI WA NYARAKA ZA UMILIKI ARDHI.


1Mmoja wa wananchi kutoka Wilaya ya Temeke (aliyesimama) akieleza kero yake kwa Mhe. Lukuvi wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi.

2William Lukuvi akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kutoa kero zao za masuala ya ardhi.
………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, amekutana na wakazi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni katika kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi. Katika mahojiano na wananchi hao, Mhe. Lukuvi amewaonya wananchi kuwa makini na matapeli wanaochukua nyaraka halali za umiliki na kutengeza nyaraka feki.
Hayo yamebainika baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia mmliki wa kampuni ya Holland Investment iliyopo  jijini Dar es Salaam kwamba, amekuwa akichukua nyaraka halali za umiliki kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia na baadae kuwabadilishia na kuwarudishia nyaraka feki.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

No comments