Header Ads

Responsive Ads Here

LIVERPOOL YAKUBALI KUTOA £40M KUMSAJILI OXLADE CHAMBERLAIN


_97610144_74c06424-7215-4440-9e7c-87ba24171827

Majogoo wa Anfield timu ya Liverpool imekubali kuilipa Arsenal dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade Chamberlain.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikataa uhamisho wa Chelsea siku ya Jumanne baada ya makubaliano kuafikiwa, atajiunga na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Oxlade Chamberlain ambaye yuko mwaka wake wa mwisho wa kandarasi na Arsenal, alikataa mkataba mpya ambao angekuwa akilipwa £ 180,000 kwa wiki katika uwanja wa Emirates huku akiwa ameanzishwa mechi zote nne za Arsenal msimu huu.
Kiungo huyo wa kati anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuelekea Malta na Uingereza siku ya Alhamisi kabla ya dirisha la uhamisho kukamilika tangu Oxlade Chamberlain ajiunge na Arsenal ameichezea klabu hiyo mara 198 tangu akitokea Southampton mnamo mwezi Agosti 2011, akifunga mabao 20.
Kitita hicho kingevunja rekodi ya usajili wa Liverpool, lakini timu hiyo imekubali kumsajili mchezaji wa RB Leipzig Naby Keita msimu ujao kwa kitita cha £48m mpaka sasa Liverpool imemsajili winga Mohammed Salah kutoka Roma kwa £34m, beki Andrew Robertson kutoka Hull kwa £8m na mshambuliaji Dominic Solanke baada ya kandarasi yake katika klabu ya Chelsea kuisha.

No comments