Header Ads

Responsive Ads Here

LISU KUTIKISA MKUTANO WA UAMSHO HAPO KESHO


4e32e93322c5fee4ca3cb0918c164582
Na Sales Malula

Mwimbaji wa nyimbo za injili John lisu pamoja no waimbaji wengine wa nyimbo za injili wanatarajia kupamba tamasha kubwa la uamsho linaloanza kesho. 

Katika mahojiano maalumu na Mtandao huu Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (victory Christian center) DK. Huruma Nkone amesema wameandaa mkutano wa uamsho unaoshirikisha watu wote bila kujali utofauti wa madhehebu hayo
Akifafananua zaidi alisema mnenaji katika mkutano huo wa uamsho ni mhubiri maarufu hapa nchini Askofu Yona Suleiman kutoka kiomboi mkoani Singida.

Mkutano huo wa uamsho utafanyika katika ukumbi Wa Kanisa la Victory Christian Center Mbezi A mwai kibaki road ambapo usafiri wa kuja Kanisani utatolewa bure kuanzia Mwenge ambapo kwa tegeta na Bunju pia usafiri utakuwepo. 
 Mkutano huo wa siku tatu yaani tarehe1-3 September 2017 saa kumi kila siku unatarajiwa kuwa wa Baraka ambapo wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam watahubiriwa na kuacha Maovu
Ni Kwa Neema Tu: Waimbaji wengine watakaopamba mkutano huo wa uamsho ni Rivers of Joy International Kwaya ya Kanisa la KLPT Tageta na nyingine nyingi.
DK Nkone ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar kujitokeza kwa wingi kwani Huduma ya maombi  na maombezi itatolewa bure.

No comments