Header Ads

Responsive Ads Here

KIKAO CHA UTENDAJI KAZI KATI YA MENEJIMENTI YA TEMESA MAMENEJA NA WAKUU WA VITUO CHAFANYIKA


PIC 1
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Utendaji Kazi kati ya Menejimenti ya Wakala, Mameneja wa Mikoa na Wakuu wa Vituo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle na kushoto ni Jonas Bakuza, Kaimu Mhasibu Mkuu wa wakala huo.

PIC 2
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Utendaji Kazi kati ya Menejimenti ya Wakala, Mameneja wa Mikoa na Wakuu wa Vituo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Wa kwanza Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Hans G. Lyimo, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle. Kushoto kwa Dkt. Mgwatu ni  Kaimu Mhasibu Mkuu wa wakala huo Jonas Bakuza na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe. Kikao hicho kilijadili Maandalizi na utekelezaji wa bajeti za Mikoa na Vituo, mabadiliko ya sheria mbalimbali pamoja na Taratibu za Ununuzi.
PIC 3
Ndugu Hans G. Lyimo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akitoa ufafanuzi wakati wa Kikao cha Utendaji Kazi Kati ya Menejimenti ya Wakala, Mameneja wa Mikoa na Wakuu wa Vituo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Wa pili Kulia ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japheth Y. Maselle, Mtendaji Mkuu wa wakala huo Dk. Mussa Mgwatu, Kaimu Mhasibu Mkuu Jonas Bakuza na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe. Kikao hicho kilijadili Maandalizi na utekelezaji wa bajeti za Mikoa na Vituo, mabadiliko ya sheria mbalimbali pamoja na Taratibu za Ununuzi.
PIC 4
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme  (TEMESA) Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Alfred Ng’wani akitoa hoja wakati wa kikao cha Utendaji Kazi kati ya Menejimenti ya Wakala, Mameneja wa Mikoa na Wakuu wa Vituo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili Maandalizi na utekelezaji wa bajeti za Mikoa na Vituo, mabadiliko ya sheria mbalimbali pamoja na Taratibu za Ununuzi.

No comments