Header Ads

Responsive Ads Here

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUUNDA KAMATI ZA ULINZI WA WATOTO KUANZIA NGAZI YA MTAA.


Pix 9
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Baraza la Watoto Taifa Lulu Nziku mara baada ya kumaliza mkutano na Baraza la kata ya mseke iringa Vijijini hivi karibuni.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) Bibi Sihaba amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri zote nchini kutekeleza wajibu wa uundaji wa Kamati za Ulinzi na Usalama wa mtoto kuanzia ngazi ya mtaa mahali walipo wananchi ili kuwa na mfumo thabiti wa kuzuia na kutoa huduma kwa watoto wanaofanyiwa ukatili.
Ameyasema hayo mapema wiki hii wakati wa kikao cha majumuhisho kwenye kilele cha safari yake ya kikazi katika kijiji cha Tanangozi, kata ya Mseke, tarafa ya Mlolo, wilaaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na kupokea taarifa za utetezi wa haki za watoto kutoka kwa Baraza la Watoto la Kata ya Mseke, Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto, na Timu ya malezi ya watoto wa Kata ya Mseke.
Ameongeza kuwa mabaraza ya watoto yakianzishwa na kuimarishwa katika ngazi za vijiji na kata yatasaidia kutoa raghiba ya watoto kujitambua, kujithamini na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili na pia kujiepusha na vishawishi vya mahusiano na wanaume katika umri mdogo.
Aidha, Katibu Mkuu aliwapongeza wajumbe wa vyombo hivyo vilivyoundwa na watoto na wazazi kuendeleza wajibu wao wa kuzuia na kutokomeza ukatili na nyanyasaji wa watoto  katika ngazi ya familia, jamii na shuleni ili kuongeza ubora wa jamii zetu katika utoaji wa haki za msingi za watoto wote katika jamii zetu.
Alisema Serikali imekamilisha mwongozo wa utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza dhidi ya wanawake na watoto hapanchioni amabo utasambazwa kwa wadau ili kutoa maelekezo fasaha ya utendaji katika maeneo ya utekelezaji wa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amesisitiza  kutumia vikundi vya malezi ya watoto na sanaa katika Kata ya Msewe, Wilaya ya Iringa Vijijini kwa kujiunga pamoja na kutumia stadi na mbinu walizonazo katika kuelimu jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kuimarisha mazingira upatikanaji wa haki na usawa kwa wototo wote.

No comments