Header Ads

Responsive Ads Here

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA DANGOTE


Picha Na 1
Mtaalam kutoka Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya  GASCO inayojihusisha na usambazaji wa gesi, Mhandisi Mwanaidi Rashid (kulia) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo Namba I cha gesi  ambapo Kiwanda cha Saruji cha Dangote kitaunganishwa na huduma hiyo kwa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.

Picha Na 2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na   Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kutoka  kulia mbele) na Mwenyekiti  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia ( wa nne kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na kamati hiyo wakati wa ziara hiyo.
Picha Na 3
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha  Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na   Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) aliyeambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara baada  ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Picha Na 4
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha  Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akielezea mafanikio na changamoto za kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti (hawapo pichani). Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja.
Picha Na 5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na   Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha  Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani ) katika kikao hicho.
Picha Na 6
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha  Dangote, Hemendra Raithatha (mbele) akielezea jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Picha Na 7
Sehemu ya wajumbe kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na watendaji wa kiwanda cha Dangote wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha  Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Picha Na 8
Kutoka kulia mbele mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo, Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Josephat Mbwambo na Kaimu Mkurugenzi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika kikao hicho.
Picha Na 9
Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Josephat Mbwambo (kulia) akinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Bajeti katika kikao hicho.
Picha Na 10
Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja akifafanua jambo katika kikao hicho.

No comments