Header Ads

Responsive Ads Here

KAMATI YA BUNGE YA MALIASILI YA NCHI YA MALAWI YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI YAIPONGEZA TANZANIA

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge la Maliasili kutoka nchini Mawawi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro jana.

 Msafara wa kamati hiyo ukiwa katika hifadhi hiyo.
 Simba wakiwa barabarani wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Hifadhi ya Mikumi.
 Pundamilia na swala wakiwa katika hifadhi hiyo.
Picha ya wananchi wakiwa na baiskeli iliyobandikwa katika hifadhi hiyo.Na Calvin Gwabara, Morogoro.

KAMATI ya Bunge ya Maliasili na mabadiliko ya tabia nchi kutoka nchini Malawi imeipongeza Serikali,Uongozi wa hifadhi za taifa TANAPA na watanzania kwa namna wanavyolinda na kuhifadhi maliasi za taifa nchini.

Pongezi hizo zilitolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Werani Chirenga walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi yenye lengo ya kujifunza na kuona namna Serikali ya Tanzania inavyopiga hatua katika kusimamia maliasili za nchi ili kupata mbinu hizo na kwenda kuzitumia pia kutatua changamoto zinazoikabili nchi yao kwenye kutunza maliasili zao.

Alisema kuwa wamejifunza mambo mengi kutokana na ziara hiyo hususani namna ambavyo Serikali imeweka sheria kali na nzuri za kusimamia maliasili na kuwaadhibu wawindaji haramu kwenye hifadhi hizo sambamba na kitendo cha TANAPA kuwa na waendesha mashitaka na wapelelezi wake wenyewe katika kukabili watu wanaokamatwa wakifanya uhalifu kwenye hifadhi zao.


Mwenyekiti huyo wa Kamati hiyo ya Bunge kutoka Malawi aliongeza kuwa moja ya mbinu ambayo imekuwa ni kivutio kikubwa kwao pi ni namna wanavyotumia mbinu mbalimbali kwenye kufanya doria kwenye hifadhi hizo na kuwakamata wawindaji haramu kwa kutumia ndege zisizo na rubani pamoja na matumizi ya Mbwa kunusa nyayo wa wahalifu hao ndani ya hifadhi na mbwa kuwapeleka hadi nyumbani kwa mhalifu huyo kwa kunusa.


"Hizi ni mbinu nzuri sana ambazo lazima na sisi Malawi tukazitumie katika kupambana na wawindaji haramu wetu maana changamoto mlizonazo nyinyi ni sawa na zilizopo kwenye nchi yetu na nchi nyingine nyingi za afrika lakini nyinyi mmefanikiwa sana na mnapaswa kupongezwa" Alisema Mhe. Chirenga.

Pia alipongeza Serikali ya Tanzania kwa kwa hatua yake ya kuipatia TANAPA fedha za kutosha kwaajili ya kuendeleza uhifadhi wa hifadhi zake kwa kurudisha fedha za makusanyo kiasi kwaajili ya kuendeleza hifadhi zake.

Hata hivyo wamesikitishwa na idadi ya wanyama wanaouwawa kila mwezi kutokana na kuwepo kwa barabara kuu  inayokatiza katikati ya hifadhi hiyo na hivyo kuunga mkono juhudi za serikali za kuichepusha barabara hiyo ili kupunguza idadi hiyo ya wanyama wanaogongwa.

Awali akitoa mada ya maelezo ya hifadhi hiyo mbele ya kamati Kaimu mkuu wa hifadhi hiyo bwana Gerald Mono amesema pamoja na mafanikio mengi ambayo hifadhi inayapata mwaka hadi mwaka lakini changamoto ya Barabara hiyo imekuwa kubwa kwani kwa takwimu za mwaka 2013 - 2016 zinaonyesha wastani wa wanyama 29 wanauwawa kwa ajali zinazotokana na barabara hiyo Kila mwezi.

Mhifadhi huyo amesema pia wastaniwa kilo 138 huokotwa kila wiki kandokando ya barabara hiyo kutokana na watumiaji wa barabara hiyo kutupa mabaki ya vyakula na takataka zingine ngumu kama mifuko ya nailoni na plastiki ambazo ni hatari kwa wanyama pale watakapozila huweza kumuua mnyama.


 Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya Ulinzi kwenye hifadhi hiyo ya Mikumi bwana Davis Mushi aliiambia Kamati hiyo ya Bunge ya Maliasili na mabadiliko ya tabia nchi kutoka Malawi kuwa mikakati madhubuti ya ulizi wa hifadhi hiyo inayotokana na matumizi ya mbinu za hali ya juu za kutumia ndege zisizo na rubani na mbinu zingine zimesaidia kupunguza kuuwawa kwa Tembo kutoka tembo watano mwaka 2010 hadi tembo mmoja mwaka 2016.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA bwana Mtango Mtahiko amesema TANAPA imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na jamii zinazozunguka hifadhi hizo ili kuendelea kusaidia kutoa ushirikino katika uhifadhi wa maliasi hizo na hujitahidi kuendesha na kusaidia miradi mbalimbali kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi kama vile ujenzi wa shule,zahanati na miradi mingine ya maendeleo.

Amesema pamoja na TANAPA kuwa na hifadhi 16 za taifa lakini ni hifadhi mbili tuu za Serengeti na Mlima Kilimanjaro ambazo zinazalisha zinaingiza fedha nyingi za kujiendesha,kuendesha hifadhi zingine pamoja na kutoa mchango kwenye pato la taifa na jitihada zinaendelea za kuhakikisha hifadhi zote zinatangazwa vizuri na kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea hifadhi hizo.

Alisema Idadi watalii imeongezeka kwenye hifadhi ya taifa ya Mikumi ambapo mwaka 2010/2011 watalii kutoka afrika mashariki walioingia ni watalii 22,971 wakati watalii wasio w afrika mashariki walikuwa 19,325 na mwaka 2015/2017  watalii kutoka ndani ya afrika mashariki waliongezeka hadi kufikia 30,262 wakati wale wa nje ya afrika mashariki walikuwa 21,240.

No comments